MBWANA SAMATTA NA JUHUDI ZA KUFIKIA MAFANIKIO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Friday, December 27, 2019

MBWANA SAMATTA NA JUHUDI ZA KUFIKIA MAFANIKIO


Mbwana Ally Samatta (alizaliwa 23 Disemba 1992) jijini Dar es salaam ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania anayecheza nafasi ya mshambuliaji katika klabu ya K.R.C Genk nchini Ubelgiji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 Ya nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba S.C. mwaka 2010, ambapo alicheza kwa nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe kutokea DRC, alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo. Mwaka 2015, alishinda taji la mcheza bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions Ligi) na kuisaidia klabu yake kshinda taji hilo.
Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji manamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi ya Ubelgiji na akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya ubelgiji (Ebony Shoe award).
Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[1]
Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja Nigeria tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[2] 
Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo (hat-trick) iliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika, magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[3]
Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aljiunga na klabu ya K.R.C Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[4] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[5]

Mbwana samatta ameweka rekodi ya kuwa mtanzania pekee aliecheza michuano ya Uefa champions ligue licha ya timu yake kutokufanya vizuri katika mashindano hayo, na alifanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo 6, historia pekee nay a kukumbukwa ni pale alipoifunga Liverpool nyumbani Anfield…………INSERTS
Mbwana Samatta wakati akiichezea simba alifunga mabao 13 katika michezo 25, na baadae Tp mazembe alifunga mabao 60 katika michezo 103, mpaka sasa Samatta ameichezea Genk michezo 98 na kufunga mabao 43, na timu ya taifa ya Tanzania michezo 56 mabao 20, jumla akifunga mabao 136 katika michezo 282.
Mei 2019 al;ishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya ubelgiji (Ebony Shoe).[6]
mpaka sasa ameshinda tuzo mbalimbali ikiwemo
ubingwa wa ubelgiji, supa cup ubelgij, ubingwa wa Tp mazembe vikombe 7, mchezaji bora wa bara la afrika, mchezaji bora wa ubelgij kwa wachezaji wenye asiri ya bara la afrika.
Mbwana samatta amemuoa mrembo Neima Mgange na kufunga nae ndoa jijini dar es salaam. Mbwana samatta ni mdogo wa mchezaji wa Kmc Mohamed Samatta ambao wote wametokea katika familia yam zee Alli Samata mchezaji wa zamani wa Balimi fc.

Nikukumbushe tuu Baba yake mbwana samatta alimpata mama samatta wakati akiwa mchezaji wa balimi fc huko mkoani kagera na mama yake samatta alikuwa askari ambae kabla ya hapo mama yake samatta alitoa ofa kwa mchezaji atakae funga bao atapata zawadi ya soda ndipo mzee Samatta alipofunga bao na kwenda kuchukua zawadi yake na hapo mahusiano yao yalipoanza chanzo kikiwa ni soda. hahahahaa

🎉 Happy Birthday, Mbwana Samatta

Makala hii imeandaliwa na Alex Mwenda Daady

No comments:

Post a Comment