RAISI SAMIA AIPA POLE SIMBA KWA KUFUNGWA MISRI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Friday, April 5, 2024

RAISI SAMIA AIPA POLE SIMBA KWA KUFUNGWA MISRI

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kwamba pamoja na kufungwa mabao 2-0 na Al Ahly usiku wa jana, lakini Simba SC ilipambana na juhudi zao zimeonekana.

“Mchezo mzuri Simba. Usiku haukuwa wa ushindi lakini tumeziona juhudi na zinatupa faraja na matarajio kuwa, msimu ujao wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika mambo yatakuwa mazuri zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha,”amesema Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Simba SC kwa mara nyingine imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika Hatua ya Robó Fainali baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Al Ahly usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.


Mabao yaliyoizamisha Simba jana yalifungwa na kiungo Amr El Soleya dakika ya 47 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mfaransa, Anthony Mbu Agogo Modeste na mshambuliaji, Mahmoud Abdelhamid Soliman dakika ya 90 na ushei.

Kwa matokeo hayo Al Ahly inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Sasa Mabingwa hao watetezi, Al Ahly na watamenyana na mshindi kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambao mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.

1 comment:

  1. Ushuhuda Wangu Kuhusu Dkt. Dawn – Mtu Aliyerejesha Nyumba Yangu na Furaha Yangu

    Nataka kushiriki ushuhuda wangu wa dhati kuhusu jinsi Dkt. Dawn alivyobadilisha maisha yangu kabisa.

    Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na alikuwa ameenda kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwangu — na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini si hayo tu — Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyokuwa ikizunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote — huzuni, bahati mbaya, au mkanganyiko — usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete