JINI MAHABATI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, March 19, 2018

JINI MAHABATI

Image may contain: 2 people, text

RIWAYA: JINI MAHABATI
SEHEMU YA 1

AGE: 18+
Mavazi ya heshima yasiyokuwa na heshima aliyokuwa akipendelea kuvaa Radhia maarufu kwa jina la Kisura yalitosha kabisa kumchanganya Tariq na kujikuta akimpenda ghafla binti huyo waliyekutana eneo la chuo kikuu cha Eckernford Tanga.Uzuri wa umbo la kibantu na wowoo au kijungu mchongoko alilojaliwa binti huyo vilimfanya mwanaume yeyote aliyekutana naye kupagawa na pengine kutaka hata kumsalimia.Mpasuo wa mbele wa gauni refu alilovaa binti huyo ulimfanya Tariq ageuke mara baada ya kupishana na binti huyo kwenye barabara hiyo ya kuingia chuoni.
Mtikisiko mtikisiko wa makalio ya binti huyo mithili ya mawimbi ya bahari ya hindi yalizidi kumchnganya Tariq na kujikuta akiumia shingo kwa kumuangalia.Uvumilivu ukamshinda akajikuata anageuka na kuanza kurudi chuoni alipotokea ili mradi apate hata nafasi ya kumsemesha binti huyo.Macho ya Tariq yaliganda kwenye sehemu za nyuma za wowooo la binti huyo ambalo licha ya ukubwa na mirindimo ya pwani pia zilionesha michirizi chirizi ya nguo ya ndani.
Tariq alilalamba lamba midomo yake kutokana na uchu mkubwa alioupata mara baada ya kugundua kuwa nguo ya ndani ya binti huyo ilikuwa ni ya pink tofauti na gauni la light blue alilokuwa amelivaa. 
Tariq alizidi kumfuata mpaka binti huyo akaingia chuoni kabisa na alikuwa akielekea moja ya ofisi hapo chuoni. Tariq alijikuta akikooa kwa nguvu jambo lilomfanya binti huyo ageuke. “Jamani huko vizuri alichombeza Tariq huku akipiga hatua za haraka haraka ili aweze kuomba namba za simu.Akajikuta anatoa kalamu na karatasi kisha kuandika namba zake za simu na kumkabidhi binti huyo.
Radhia alitabasamu kisha akazichukua zile namba na kuingia ofisini. “Sijui ni msubiri au niondoke zangu” Tariq alijiuliza mara baada ya kutoa namba zake na kubaki hapo nje.”Any way kwa kuwa nimeshampa namba zangu wacha mimi niende zangu” Tariq alijijibu.
Radhia aliingia ofisini kwa lengo la kukamilisha udaili wa kujiunga na chuo kikuu cha Enckernford Tanga kwa sababu alikuwa amechelewa na mda wa usahili ulikuwa umeisha.Alichelewa kutokana na mvutano na familia yake ambayo haukupenda binti huyo kusoma nje ya jiji la Dar es salaam na walikuwa wako tayari kutumia gharama yeyote kuhakikisha kuwa binti huyo anapangiwa vyuo vilivyopo Dar es salaaam...
Radhia ni mtoto wa balozi mstaafu na mama yake anafanya kazi kama katibuu mkuu wa wizara moja hapa nchini.Radhia ameishi kwenye mazingira mazuri sana na sasa anafuraha sana maana atapata uhuru wa kuishi maisha yake kuacha yale ya kubanwabanwa aliyokuwa akiishi tangia akiwiwa mdogo.Radhia au Kisura jina alilopewa akiwa sekondari alipenda sana kwenda kusoma mbali na Dar es Salaaam ili aweze kupata uhuru wa kuishi maisha ayependayo tofauti na yale ya kubanwabanwa na wazazi wake.Hivyo hata katika uchaguzi wa vyuo alijaza vyuo vya nje ya Dar es salaam hivyo kupelekea kupangiwa Tanga jambo ambalo halikuwafurahisha wazazi wake.
Alipoingia tu ofisini harufu ya marashi ya kunukia ilimshitua mwalimu aliyekuwa akihusika na kukamilisha usaili kwa wanafunzi waliochewa.Macho ya tamaa ya kiume yaliangukia kwenye matiti ya binti huyu ambayo yalikuwa ni makubwa na yameachiwa huku kukiwa na kitatoo kidogo cha makopa kwenye titi lakushoto. “Karibu alijikaza na kusema Mwalimu huyo mara baada ya kugundua kuwa binti aliyeingia ofisi alikuwa na urembo uliopitiliza”.
“Asante Radhia alijibu kwa sauti iliyojaa mbwembwe na kila ishara ya ushawishi kuwa yeye ni mrembo. Ule mpasuo wa gauni alilovaa binti huyu vilimfanya mwalimu huyo aendelee kumshangaa na kumezea mate kama simba aliyeona swala.Basi Radhia alieleza shida yake na kutokana na muonekano wake alisikilizwa na kusaidiwa akakamilisha mchakato huo,akaaga na kuondoka na wakati anapiga hatua kuondoka yule mwalimu alimwita na kumwambia mbona hujaandika namba yako ya simu? Radhia akamuangalia kwa madaha kisha akatabasamu na kumwambia mbona sijaona sehemu ya kuandika namba”? “Ok hii form yako itakuwa imekosewa” alijiuma uma mwamlimu huyo. “Kwa hiyo nifanyaje aliuliza Radhia kwa kujiamini? “Andika namba yako kwa juu"mwalimu alijibu huku akizidui kumshangaa.
Radhia aliaandika namba kisha akotoka zake na kuondoka. “Yaani huyu mwalimu aseme tu amedata na mimi na alitaka namba zangu sio eti form imekosewa” aliwaza Radhia huku akiwa anaondoka.Aliondoka na alipofika getini alikodi tax na kumpeleaka mahali alipokuwa anakaa.
Yaani wangejua kuwa mimi na uzuri wote huu mpaka sa hivi sijaguswa ni bikira hata wasinge angaika na mimi.Ila safari hii sijui kama nitaweza kujizuia maana nitakuwa huru kabisa na wazazi waliokuwa wakinilinda watakuwa mbali aliwaza Radhia na kuingia Chumbani kwake, chumba alichokodisha mara baada ya kukosa hostel kwa sababu alichelewa kuripoti chuoni.*************
Pangani mkoani Tanga miaka mingi sana iliyopita kuliwahi kutokea binti mzuri sana na mwenye umbo na sura kama ya Radhia.Binti huyu maarufu alijulikana kwa jina la Barike.Inasemekana binti huyo alikuwa ni mwanamke mzuri sana, mwenye mwendo wa madaha , mwendo uletao raha mwendo usio na karaha mwendo wa kuvutia kila alipojaribu kupiga hatua.Alikuwa kama mwarabu mwenye rangi ya dhahabu na hasiye na ghadhabu na pia alipenda kuvaa magauni marefu kama hayo apendayo kuvaa Radhia.Basi binti huyo alikuwa akitokea kwenye familia ya kitajiri na baba yake alikuwa ni Mwinyi au unaweza kusema Chifu katika mjini huo wa Pangani.
Siku moja binti huyu alikwenda kuoga sehemu maarufu ambayo huwa wanaitumia kuoga na kufanya matambiko.Sehemu hiyo kuna rasi ambayo ukiingia kuna mlango wa kutokea Unguja.Basi binti huyo alikuwa na mfanyakazi wao na kwa bahati mbaya alikuwa kwenye siku zake za hedhi.Basi walioga na walipomaliza walianza kusukana huku wakibarizi na kupunga upepo.Ghafla kulitokea tukio la ajabu sana katika historia ya mji huo kwani binti yule alibadilika na kuwa jiwe.Kwa mujibu wa wakazi wa huko walidaikuwa binti huyo alifanya makosa makubwa kwenda kuoga katika sehemu hiyo yenye kuheshimika akiwa katika siku zake za mwisho wa mwezi.*****ITAENDELEA****

No comments:

Post a Comment