Paris St-Germain wako tayari kulipa pauni milioni 111.5 ili kumsajili mshambuliaji wa tumu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen, 25, kutoka Napoli msimu huu. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Chelsea wanaendelea kutafuta mshambuliaji mbadala wa Osimhen, huku mchezaji wa kimataifa wa Ukraine na Girona Artem Dovbyk, 26, akiwa kwenye rada za klabu hiyo. (GiveMeSport)
Manchester United wanapanga msimu ujao huku Erik ten Hag akiwa meneja wa klabu hiyo kwa muda kutokana na kukosekana kwa mbadala wake. (i news)
Manchester City wamekubali dili la kumsajili winga wa Troyes Mbrazil Savio, 19, ambaye yuko Girona kwa mkopo. (Football Insider)
Manchester United wanapanga msimu ujao na Erik ten Hag kama kocha walau kwa muda mfupi.
Mahitaji ya Manchester United ya kutaka ada ya pauni milioni 34 kwa ajili ya Jadon Sancho yanaweza kukatiza hamu ya winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 kutaka kurejea kwa mkopo Borussia Dortmund kuwa wa kudumu. (Sky Sport - kwa Kijerumani)
Kocha wa Sporting Lisbon anayenyatiwa na Liverpool Mreno Ruben Amorim, 39, amekiri kuwa "hawezi kukuthibitisha" kuwa atakuwa mkufunzi wa klabu hiyo msimu ujao. (ESPN)
Amorim ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 12.8 katika klabu ya Sporting msimu huu wa joto, ambacho kitashuka hadi pauni milioni 8.5 mwaka wa 2025. (Sun)
Chelsea haitazingatia ofa za kumnunua beki wa Uingereza Reece James, 24, msimu huu licha ya tetesi zinazomhusisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 na PSG au Real Madrid. (Football Insider)
Eddie Howe ameelezea azma yake ya kumbakisha Bruno Guimaraes Newcastle huku Magpies wakijiandaa kuzuia klabu nyingine kumnunua kiungo huyo wa Brazil, 26, kutoka PSG. (Mirror)
Manchester City wako tayari kupata hasara kubwa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, msimu huu. (Football Insider)Tottenham wanapania kumnunua kiungo wa Leicester City Kiernan Dewsbury-Hall, 25, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa pauni milioni 25 ikiwa Foxes watashindwa kupanda daraja kurejea Premier League. (Talksport)
Mshambulizi asiyetakikana wa Barcelona Ansu Fati, 21, hatarejea Brighton msimu ujao - lakini Wolves, Sevilla na Valencia wote wanafikiria kumnunua mshambuliaji huyo wa Uhispania kwa mkopo. (Sport - kwa Kihispania)
Burnley wamekubali mkataba wa kumsaini beki wa Uholanzi chini ya umri wa miaka 21 Shurandy Sambo msimu wa joto mara baada ya mkataba wa mchezaji huyo wa PSV Eindhoven kumalizika. (Fabrizio Romano)
Leeds United itaweka kipaumbele usajili wa kudumu wa beki wa Wales Joe Rodon, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea Tottenham, iwapo watapandishwa daraja hadi Ligi ya Premia. (Football Insider)
Beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 29, anataka tu kuichezea Barcelona msimu ujao licha ya vilabu vingine kumtaka. (Sport - kwa Kihispania)
No comments:
Post a Comment