JINI MAHABA SEHEMU YA PILI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, March 19, 2018

JINI MAHABA SEHEMU YA PILI

pd_sex_070731_ms
RIWAYA: JINI MAHABATI
SEHEMU YA 2

AGE: 18+
ILIPOISHIA
Siku moja binti huyu alikwenda kuoga sehemu maarufu ambayo huwa wanaitumia kuoga na kufanya matambiko.Sehemu hiyo kuna rasi ambayo ukiingia kuna mlango wa kutokea Unguja.Basi binti huyo alikuwa na mfanyakazi wao na kwa bahati mbaya alikuwa kwenye siku zake za hedhi.Basi walioga na walipomaliza walianza kusukana huku wakibarizi na kupunga upepo.Ghafla kulitokea tukio la ajabu sana katika historia ya mji huo kwani binti yule alibadilika na kuwa jiwe.Kwa mujibu wa wakazi wa huko walidaikuwa binti huyo alifanya makosa makubwa kwenda kuoga katika sehemu hiyo yenye kuheshimika akiwa katika siku zake za mwisho wa mwezi.*****
TIRIRIKA NAYO
Baadaye miaka mingi ilivyopita akaja akatokea tena binti mzuri mfanowe wa yule Barike aliyekufa kwenye mazingira ya kutatanisha.Binti huyo hakuwa Barike bali ni jini ambalo likuwa likiwalaghai watu na kuwaingiza matatani.Wanaume wengi sana walikufa hasa wale waliokuwa na tamaaa ya kumtokea, kumtongoza na kuomba kuonjeshwa utamu.Baadaye watu walivyokuja kushituka shetani huyo ambaye alifafana na Barike alikuja kupotea na watu wakamsahau.
Kama tujuavyo majini ni viumbe waliopewa uwezo mkubwa sana kuliko wanadamu.Mizimu yao uishi miaka mingi sana na pengine kuwaingia watu mbalimbali na kuwafanya watumwa.Mzimu huo wa Barike ndio ulimuiingia Radhia akiwa usingizini mara baada ya kukamilisha michakato yake ya kujiunga na chuo.Mzimu huo lilimwingia binti huyo kwa lengo moja tu kwamba limtumie awe anafanya mapenzi na wanaume wengi kadiri awezavyo ili wao wapate manii za wanaume ambazo wangezitumia kwa mambo yao ya kijinijini. Maninii hizo zingechukuliwa kimiujiza na baadaye kupandikizwa kwa baadhi ya wanawake ambo walipotea kwenye mazingira ya kutatanisha katika miji mbali mbali ya nchi za aAfrika mashariki ususani nchi za pembezoni mwa bahari.
Tofauti na tulivyozoea kuwa jini mahaba la kiume ndo umwingia mwanamke na huwa linamsababishia matatizo mengi na kumfanya hashindwe kuolewa hili nia yake ilikuawa ni tofauti kabisa lenyewe ni kumtia mvuto zaidi ili aweze kufanya mapenzi kadiri awezavyo na wao kujipatia manii ambazo baadaye zingepelekea wao kupata watoto ambao wangetumika kuingiza utwala wa kijini katika nchi hizo za mashariki mwa bara la Afrika .Mzimu huu wa Barike uliamua kumwiingilia Radhia kwa sababu alikuwa ni mrembo sana hivyo angeweza kuwashawishi wanaume kiurahisi.Pia kazi hiyo ilitakiwa ifanywe na mwanamke ambaye ni bikira.
Kwa kile kilichoitwa kutimiza masharti ya kikao chao cha wakati wa jua kuzama Jini Barike alipewa jukumu hilo la kutafuta binti mrembo na kumwingia.Tofauti na zamani ambapo jini hilo lilikuwa likiwalaghai wanauume na kuwatia hatiani ikiwa ni pamoja na kuwakatisha uhai sa hivi walikuja na mbinu ya mda mrefu.Waliamini kama watapata manii za wanaume basi wangeweza kuzipandikiza kwa majini wa kike kisha kuzaa watoto machotara ambao wangetumika kuingiza utawala wao wa kijini miongoni mwa wanadamu.Basi Jini Barike alianza kazi na kwa uwezo mkubwa waliopewa viumbe hao mzimu wa jinni huo uliweza kugundua kuwa katika chuo cha Eckernford kuna binti mrembo anayeitwa Radhia.***
Usiku wa siku hiyo Radhia aliota ndoto ambayo hakuielewa.Aliota kama mtu aliyekuwa akifanya mapenzi na mwanaume aliyempenda sana.Lakini kwa kuwa hakuwahi kufanya mapenzi alianza kupata uchungu mkali mara baada ya mwanaume huyo kumwingilia.Maumivu hayo makali yalimfanya Radhia kushituka kutoka usingizini. Alipigwa na butwaa mara baada ya kukuta shuka jeupe alilotandika limelowa damu. “Hii ni ndoto au ni kweli?” Radhia alijuliza huku akijikagua sehemu zake za siri” .
“Ooooooops ooooooh my God what is this?”,Radhia alilalamika mara baada ya kuhisi kuna mwanaume alimwingilia.
“Sasa atakuwa ni nani mbona na milango imefungwa?” Radhia aliwaza kabla ya kukimbilia bafuni na kujimwagia maji na kujisafisha vizuri.Akajisafisha vizuri na kurudi kulala.Wakati analala akaanza kusikia harufu nzuri ya marashi ambayo yalikuwa yakivutia sana kwenye pua zozote za mwanadamu.Si hivyo tu bali ulipulizia upepo mwanana utazani alikuwa ufukweni.Radhia akabaki anashangaa kabla ya kuamua kubadilisha yale mashuka yaliyokuwa yametapakaa damu. “Au itakuwa ni damu ya hedhi?” Radhiaalijiuliza huku ile harufu ya marashi ikiendelea kunukia.
“Hapana lakini damu ya siku zangu huwa haiwi hivi” Radhia alijijibu na kuhisi kabisa atakuwa amepoteza bikira yake kwenye mazingira ya kutatanisha.Akajipa ujasiri wa kike kisha akabadilisha mashuka na kuweka mengine kisha akapanda kitandani na kulala.Alilala kwa wasiwasi sana siku hiyo kabla ya kupata usingizi na kumwota yule kijana aliyekutana naye kule chuoni yaani Tariq.Aliota amezama kwenye penzi zito la kijana huyo lakini wakawa wanapishana sana kauli kwa sababu kijana huyo alisema kuwa Radhia sio yule wa mwanzoni bali ni jini tena jinni mahabati.
Ndoto hiyo inampeleka Radhia mpaka kwenye viumbe vya ajabu na kuonesha kuwa kweli hata yeye si binadamu wa kawaida maana aliweza kuwaelewa viumbe hivyo. “Lakini hata Tariq na yeye basi atakuwa ni jini ameyajuaje mambo haya yote na kunileta huku” aliwaza Radhia..Aliaamka huku akihisi kabisa kulikuwa na maumivu makali sana sehemu zake za siri. Ilikuwa ni tayari asubuhi na alikuta kuna barua kwenye meza yake iliyosomeka hivi. “Hongera sana Radhia umekuwa miongoni mwa viumbe wenye uwezo wa kibinadamu na pia uwezo wa kimalaika” kwa kusoma tu ujumbe huu ni kwamba umeridhia, kama lilivyo jina lako Radhia maana yake huu radhi na umeridhia au umeridhiwa.Baada ya kumaliza kusoma tu hicho kikaratasi kikapeperuka na kupotea hapo hapo chumbani.
“Mungu wangu mbona si elewe elewi aliwaza Radhia huku akifungua mlango wake.Akatoka nje kama mtu aliyechachawa kabla ya kurudi ndani na kujiandaa kwa kwenda chuoni.Alifika chuoni na kuendelea na masomo japo mawazo ya ndoto ile yalikuwa bado yakimchanganya sana akajikuta anaamua kuacha vipindi na kurudi zake hosteli.Alihisi mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wake.Alikwenda moja kwa moja kwenye kioo na kujiangalia.Radhia alizidi kujishangaa kwa sababu kulikuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wake. “Jamani mbona nimezidi kuwa mrembo hata yale madoa madoa ya chunusi siyaoni tena” alijkuta akijuiliza na kujishangaa. “Khaa!! yaani ngozi yangu imelainika na kuwa laini kama ya mtoto mdogo alizidi kupagawa na hasiamini kama kweli huyo anayejiona kwenye kioo ni yeye.
Basi hiyo siku ikaisha huku akishinda ndani akiangalia movie huku kioo kikiwa pembeni yake na kila baada ya mda fulani alikuwa akijiangalia.Hatimaye usiku ukainga akatafuta chakula cha kununua nje kidogo ya hostel hiyo akarudi zake ndani akala na kulala.Usiku kama kawaida akaanza tena kuota ndoto za mapenzi.Safari hii aliota akifanya mapenzi na yule mwalimu wa usaili yule ambaye alichachawa na kupagawa alipomwona binti huyo.Si unakumbuka mwalimu mpaka akajikuta akiomba namba za Radhia kwa kisingizio kuwa fomu yake ilikuwa imekosewa.Ndoto ikawa tamu sana na akajikuta anapiga kelele za kimahaba.
Radhia alikuwa ulimwengu mwingne sana ambao kelele zake zilifika mpaka kwenye vyumba vya wapangaji wengine.Utamu huo wa ndoto baadaye ulimshtua binti huyo na akaamka na kama kawaida yake alikimbilia bafuni kwenda kuoga.Akajisafisha vizuri huku akijiuliza kwa nini tangia aanze kuishi kwenye nyumba hiyo kuna mambo ambayo hayaelewi.
Akaamua kupotezea na kupanda kitandani na kulala.Alipojifunika shuka tu alisikia kama mtu anagonga mlango. “Eeeh atakuwa ni nani tena usiku huu aliwaza Radhia na kuinuka na kusogea mlangoni. “Wewe binti vipi kuna usalama? ilikuwa ni sauti ya baba mwenye nyumba”. “Mimi hata sielewi” alijibu Razia kwa upole. “Ebu fungua kwanza tujue ni nini kinaendelea” aliendelea kusema baba mwenye nyumba.Radhia hama binti kisuara akavuta shuka lake akajitanda vizuri maana alikuwa uchi wa mnyama.Akafungua mlango akakutana na baba mwenye nyumba ambaye na yeye alikuwa amejifunga taulo tu.
Mwanga wa taa wa chumba cha Radhia ulitosha kabisa kufanya baadhi ya mautamu yake kuonekana na mzee baba mwenye nyumba alijikuta akilamba lamba midomo yake kwa uchu wa tamaa mara baada ya kuona jinsi binti huyo alivyokuwa amejaliwa vitu hadimu.”Nimesikia kama unapiga kelele za mtu kukubaka na nimesikia kabisa unasema unabakwa” aliuliza baba huyo huku akijitahidi kurudisha mtarimbo wake pembeni ambao ulishasimama na kuanza kuleta fujo.**ITAENDELEA**

No comments:

Post a Comment