HISTORIA YA MIRAJ ATHUMAN MADENGE SHEVA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Friday, December 27, 2019

HISTORIA YA MIRAJ ATHUMAN MADENGE SHEVA


Miraj Athuman Madenge Sheva winga wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya simba, alizaliwa desember 27 1993 jijini Dar es salaam katika familia ya mzee Madenge.Taswira inaweza kujumuisha: Mtu 1, kusimama, viatu, mtoto na nje
Alianza kujihusisha na masuala ya soka wakati akiwa shule ya msingi na sekondari ambao rasmi aliingia katika soka na kuitumikia timu ya Sifa united yenye maskani yake jijini Dar es saalam.
Baada ya kuonesha uwezo mzuri akasajiliwa na simba B ambapo pia hakudumu klabuni hapo na kuamua kutafuta maisha sehemu nyingi alipotimkia Toto afrika ya mwanza mwaka 2015.
Baada ya msimu mzuri klabuni hapo akatimkia Afrika lyon ambapo napo hakudumu sana, baada ya timu hiyo kushuka daraja nae alitimka klabuni hapo.
Alionesha uwezo mzuri wa kufumania nyavu licha ya kikosi hicho kuonekana dhaifu ndio Simba walipomtwaa kwa mara nyingine. Hakupata nafasi katika kikosi cha wakubwa na kuamua kutimkia Mwadui fc ya mkoani Shinyanga ambapo kule nako aliuwasha moto kiasi cha kuvitoa udenda vilabu vya simba na yanga.
Msimu wa mwaka 2018]2019 aliamua kwenda kujiunga na Lipuli fc ya mkoani Iringa ambapo alionesha uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na kuvitamanisha tena vilabu vikubwa, alitengeneza safu bora ya ushambuliaji ndani ya Lipuli ikiongozwa na Paul Nonga, Haruna shamte, daluesh saliboko pamoja na jimmy shoji mwaisondola, na kuiwezesha Lipuli fc kucheza fainali ya FA na kupoteza dhidi ya Azam fc.


Alex Mwenda Daady ambae ni mwaandaaji wa Makala hii anaendelea kumwangazia Miraji Athuman ambae alisajiliwa simba kimya kimya bila mbwembwe zozote zile.
Alionekana katika mchezo wa kwanza wa kirafiki wa Simba vs Gwambina fc akivaa uzi mwekundu ndipo alipozua maneno kwa mashabiki wakihofia uzoefu wake kama atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba.
Na hatimane Simba day jina La miraji Athumani likatajwa.
Baada ya kutua klabu hapo ndipo moto ulipoanza kuwaka kwa upande wake, mechi ya kwanza dhidi ya Jkt tz akitokea benchi alifunga bao la tatu assint saf ya meddie kagere, simba ikisha bao 3-1.
Katika mchezo wa pili akitoa benchi tena ndie aliekwenda kufunga bao la ushindi vs Mtibwa sugar simba ikiibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Hapo ndipo moto wake rasmi ulipowaka akicheza mechi dhdi ya kagera licha ya kutofunga aliiisadia timu kutengeneza bao baada ya kuangushwa ndani ya 18.
Na akazidi kufunga na kufunga. Miraj Athuman sheva ndie mchezaji bora wa ligi kuu nchini kwa mwezi September, alipowashinda meddie kagere na ismail kada wa tz prisons.
Happy birthday Miraj Athuman Madenge aka Sheva kwa kutimiza miaka 26 hii leo.
Makala hii imeandaliwa na Alex Mwenda Daady

No comments:

Post a Comment