SIMBA KUWAFARIJI YANGA WATAKAPOTUPA KARATA YAO YA KWANZA SPORTPESA CUP LEO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, June 4, 2018

SIMBA KUWAFARIJI YANGA WATAKAPOTUPA KARATA YAO YA KWANZA SPORTPESA CUP LEO




kikikosi cha Simba SC leo kinaanza kutupa karata yake ya kwanza katika michuano ya SportPesa Super Cup iliyoanza jana mjini Nakuru nchini Kenya.

Simba itakuwa ina kibarua dhidi ya Kariobang Sharks ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa tisa alasiri.

Kuelekea mechi hiyo, Simba wamedhamiria kupigania matokeo chanya huku wakiahidi kutokufanya vibaya kama ilivyokuwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, amesema wameamua kuiwekea msisitizo awamu hii michuano hiyo ili kupata nafasi ya kucheza na Everton huko Goodison Park, England, na hii ni endapo watakuwa mabingwa.

Kufanya vizuri kwa Simba leo kutakuwa kunawafariji watani zake wa jadi Yanga waliotolewa jana na KK HomeBoys pamoja na JKU iliyoondoshwa na Gor Mahia FC.

Ikumbukwe katika mashindano hayo yaliyfanyika Dar es Salaam mwaka jana, Simba na Yanga walitumia wachezaji wa kikosi cha pili na badala yake wakashindwa kukitwaa kikombe kilichochukuliwa na Gor Mahia FC.

No comments:

Post a Comment