BONDIA BENSON MWAKYEMBE ANGEKUA ULAYA SURA YA ANTONY JOSHUA INGEKUA ICU - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, January 17, 2019

BONDIA BENSON MWAKYEMBE ANGEKUA ULAYA SURA YA ANTONY JOSHUA INGEKUA ICU

Tunapozungumzia suala la mashujaa ulimwenguni basi tunawaangaza mashujaa wengi sana Chief Songea, Kinjikitile Ngware, Chief Mkwawa, chief Milambo, Mwalimu Nyerere, Kwame Nkruma, tukija katika ngazi za michezo wapo kina Stivin Mapunda, King Kibaden, Salvatory Edward, mtemi Ramadhan na mashujaa wengi ambao walitamba katika ulimwengu wa soka hapa Tanzania.

Turudi katika upande wa masumbwi wapo mabondia wengi sana ambao walifanya vizuri katika mapambano hapo aaaah namkumbuka Snake boy, Fransis Cheka, marehemu Thomas Mashari, nawakumbuka na mawandondi wengi sana ambao walifanya vizuri sana.

Hapa mkoani Ruvuma tunao wanandondi wachache ambao wanafanya vizuri katika ulimwengu wa mapigano,  Mussa Omary, Roy Mbunda, lakini shujaa wa Keysports kwa siku hii ya leo ni Benson Mwakyembe, uwiiiiii huyu jamaakama angezaliwa marekani tungemfananisha na Froyd Mayweather, au hata Mohameid Ali..

Katika michezo yote hapa mkoani Ruvuma ambayo ilikuwa inaitangaza vizuri mkoa wetu basi ni mchezo wa ngumi, hivi ninyi viongozi wa chama cha ngumi hapa mkoani Ruvuma mnasimamia kweli kwa nafasi mliyojiweka? inasikitisha sana kwa mtu kama Benson Mwakyembe mwanamasumbwi bora sana hapa Ruvuma na Afrika mashariki yote  lakini macho yenu kama hayamtazami hivi na ubora wake, leo hii Benson Mwakyembe ni mtu wa kufanya kazi za kukatisha watu tiketi kweli????

Image result for benson mwakyembe
Mmesahau alivyoitangaza vizuri mkoa wa Ruvuma katika masumbwi, mnakumbuka alivyopata ushindi mbele ya Mkenya 2013, mmesahau  kabisa mara ya mwisho alipata ushindi tena hapa hapa Ruvuma uwanja wa majimaji, yote hayo mmesahau na mnachofurahia ni kuona kipaji cha kijana huyu kikiwa kinadidimia katika ardhi isiyo na msaada…..

Ni aibu kubwa sana kwa chama cha ngumi mkoani Ruvuma kushindwa kuwaandaa madondia haya wazuri, mnashindwa hata kutafuta udhamini wa kusimamia mchezo huu??? kuna haja gani sasa ya kuwepo kwa chama cha ngumi na kama kipo kinafanya kazi gani,,,,tuendelee kusubili tuu mpaka Kaike promotions amwandalie pambano Benson Mwakyembe, apate matokeo mazuri Wanaruvuma tujivunie…

Hapa ndo napowaza kwanini Alexx Mwenda anapenda masumbwi lakini haingii kucheza na anabaki kuwa shabiki wa Antony Joshua ndipo napopata majibu yake….Benson Mwakyembe wewe ndio shujaa wetu wa leo ndani ya keysports tunaojua ngumi tunatambua uwepo mchango wako, na tunaomba makampuni mbalimbali wajitokeze kudhamini mchezo huu wa masumbwi ili siku moja tuwaone wanamasumbwi wetu katika ubora wa kimataifa…..

Usijutie Benson kuzaliwa Tanzania na kukulia arhi ya Ruvuma, hata Alex Mwenda anatamani angezaliwa Marekani ambao wanajua namna ya kuvitumia vipaji vya masumbwi, lakini apambane na hali yake kwasababu tayari alishazaliwa hapa Tanzania……

Wanaruvuma kwa pamoja tushirikiane taasisi binafsi, makampuni mbalimbali, wafanya biashara tuandae pambano katika mkoa wetu wa Ruvuma, tusibaki kushabikia pambano la Fransisi Cheka na Abdalah Pazi Dulla mbabe, kwa pamoja tunaweza…..
Huyu ndie Benson Mwakyembe shujaa ambae  anapotezwa na kipaji chake katika ramani ya masumbwi

No comments:

Post a Comment