SHUJAA WA KEYSPORTS LEO TUNAMWANGAZIA BONDIA Floyd Myweather - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, January 14, 2019

SHUJAA WA KEYSPORTS LEO TUNAMWANGAZIA BONDIA Floyd Myweather


MAYWEATHER
Image result for mayweather
Imeandaliwa na Alex Mwenda-Songea
Wazazi wengi huwasisitiza vijana wao wasome ili waje kuwa na maisha bora hapo baadae huku imani ikiwatuma kusoma ndio mtaji mzuri wa maisha hapo baadae. Hapa Tanzania siasa ndo kitu chenye kuleta manufaa zaidi. Lakini kwa shujaa wetu wa hii leo mambo ni tofauti hajui kusoma wala kuandika ila ngumi yake ikitua kichwani inaondoka na ubongo na ndie tajiri zaidi duniani kwa upande wa mapambano.
Jina lake halisi anaitwa Floyd Joy Sinclair lakini wengi wanamfahamu kwa jina la Floyd Myweather alizaliwa Februari 24, 1977 huko Grand RapidMichigan nchini Marekani kutoka kwa mama, Deborah Sinclair na baba yake Floyd Mayweather Sir.
                                                                                 
Ana urefu wa futi 5 na nchi 8 na uzito wa kilo 68.5, akiwa ni bondia mwenye rekodi ya aina yake katika masumbwi ya uzito wa Middle Weight na Super Feather Weight.
Mpaka sasa ameshashiriki mapambano 50, hajapoteza pambano hata moja, na kati ya hayo, 27 ameshinda kwa ‘knock out’, huku akitwaa mikanda 15 ya ngazi ya dunia, mitano kati ya hiyo akiishikilia kwa miaka minne mfululizo.

Mayweather ameingia katika rekodi ya mabondia wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi kwa mwaka, pambano lake la mwaka 2015, alilipwa bilioni16.5 kapambana na Man Pacq-yao, alimpiga bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao mwenye urefu wa futi tano na nchi 5, na uzito kilo 66, baada ya kuibuka mshindi katika pambano hilo mashabiki walimpachika jina la The Best Ever.

Mayweather anamiliki jeti au ndege binafisi aina ya  GulfStream GV aliyoinunua kwa gharama ya Sh4.2 bilioni. Ndege hiyo ina uwezo wa kuwabeba abiria 18, ambao huwa wanaunda timu yake ya 'The Money Team’.

Aidha  Boksa huyu ana magari ya kutosha zaidi zikiwa za  kifahari na zenye bei ya juu. Mayweather ana zaidi ya magari 10 yenye bei mbaya. Kutokana na idadi kubwa ya magari aliyonayo, amezitengea mitaa mbalimbali ya kutanua nazo.

Kuna zile za Las Vegas Collection anakoishi ambazo zote ni za ragi nyeupe, kuna zile za Miami Collection anakopenda kwenda kujivinjari ambazo zote ni za rangi nyeusi, kuna pia Los Angeles Collection na zingine kibao.
Gari lake la kwanza alilinunua akiwa na umri wa miaka 19 1996 Mercedes Benz shilingi za kitanzania milioni 600 ambayo anamiliki hadi leo. Ila kati ya zile anazopenda sana ni Bugatti zake tatu ambazo alinunua kila moja kwa kitita cha Sh203 milioni.

Bondia huyu anamiliki majumba kadhaa anazokodisha katika miji ya New York, Los Angeles, Las Vegas na Miami. Mwaka jana aliuza mojawepo ya majumba yake inayopatikana Miami kwa kitita cha Sh238 milioni. Makao yake yanapatikana Las Vegas anakoishi kwenye jumba la thamani ya Sh824 milioni

 Kila anapoona saa iliyomvutia lazima atainunua kwa gharama yeyote ile. Anamiliki saa zadi ya 20 zenye bei mbaya, zinazozidi hata kodi ya nyumba. Kati ya saa hizo adimu kuna aina ya Piaget Galaxy aliyonunua kwa kima cha Sh91.5 milioni, Audemar Piguet Royal Oak Sh119 milioni na Jacob & Co. Rainbow Tourbillon Sh183 milioni

 Hivi majuzi Mayweather alitangaza kuwa hutumia kiasi cha Sh400,0000 kununua chakula chake cha kila siku. Aidha anatumia kitita kingine cha Sh25 milioni kumlipa mpishi mmoja kwa jina Chef Q anayehusika kumwandalia mlo kwa mwaka. Aidha mpishi huyo Chef Q anadai kuwa hatozi kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa mapishi yake ila ni Mayweather ndiye aliyemsisitizia malipo hayo ambayo kwa sasa Chef Q Ndie mpishi wa ndani tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa bilioni 8 sawa kabisa Diamond platnumz.

Myweather bado ni mtu ambae kila kila kwake ni hela hela tu mwaka 2015 Alipokuwa akitia sahihi mkataba wake wa pigano dhidi ya Manny paqyao, Floyd alitumia kalamu ya dhahabu kwa jina 'Peerless’ yenye thamani ya Sh366,000. Kalamu hiyo ilitengenezwa na vipande 18 vya dhahabu.

Kalamu hiyo inamilikiwa na watu 124 pekee kote duniani akiwemo aliekuwa Rais wa zamani wa  Marekani Barrack Obama na mtangazaji mashuhuri na mwanamke mweusi tajiri zaidi duniani Oprah Winfrey.

Kila mwaka Mayweather hutumia kiasi cha Sh549,000 kununua nguo zake za ndani pekee na kila anapovaa hazirudii tena yeye huzivua na kuzitupa. Viatu vile vile havai mara mbili hata anapokuwa kwenye ziara za nje, anapoondoka hoteli yeye huviacha kwa wahudumu wa hotelini.

FAMILIA ya Floyd Mayweather kwa hapa nyumbani unaweza kuifananisha kabisa na ile ya Matumla, iliyojaa mabondia wengi wenye vipaji kuanzia babu, baba hadi wajukuu na ikiwezekana hata kina dada.

Mayweather Jr ndiye bondia mwenye uwezo mkubwa kuliko wengine wote hadi sasa kwa kuwa hajapigwa hata pambano moja. kwa KO.

Mayweather ni bilionea ambaye utajiri wake sasa unafikia dola milioni 500 alizopata kupitia mchezo wa ngumi na hasa za kulipwa kabla ya pambano la jana alfajiri. Lakini mkali huyo anayetokea Las Vegas, Nevada nchini Marekani amewekeza kwenye maisha ya kifahari zaidi.

Ni kati ya wanandondi wenye urafiki mkubwa na wasanii mbalimbali wa muziki na waigizaji kutoka Hollywood nchini Marekani.
Kwa sasa Justin Beiber na Lil Wayne ndiyo watu wake wa karibu zaidi. Awali alikuwa rafiki wa karibu wa 50 Cent lakini ilielezwa walitibuana sababu ya kugombea mwanamke na 50 cent ndiye alishikwa kwa usaliti.

Pamoja na utajiri wake mkubwa, Mayweather amekuwa akisisitiza kwamba kamwe maisha yake hayajawa rahisi kama watu wengi wanavyofikiri na mara nyingi amemlaumu baba yake mzazi, Mayweather Sr hadharani kuwa amekuwa tatizo.

Mayweather amewahi kutumia madawa ya kulevya kama ilivyo kwa mama yake na baba yake pia ambaye alikuwa muuzaji mkubwa na amekuwa akikubali kweli aliuza kwa lengo la kuisaidia familia yake na hata Mayweather alikuwa akipata fungu lake.

Bondia huyu ambaye pia ni mjasiriamali ana miliki akaunti moja ya benki yenye zaidi ya dola milioni 600 ndani yake, na hakuna anaeijua nambari ya siri ya account yake ya mabilioni hayo zaidi ya bibi yake ambae ndie aliegundua kipaji chake cha mapigano, na kwa sasa bibi huyo ni marehemu.
                   
Mayweather ni kiongozi wa kundi liitwalo The Money Team (T.M.T), na upande wa pili wa maisha ya kimapenzi,  bado hajaoa hadi sasa ila ni baba wa watoto wanne kwa wanawake tofauti, mpenzi wake wa awali Jossie Harris amezaa naye watoto wawili wa kiume Koraun na Zion, na mmoja wa kike anayeitwa Jirah.
                                                                      
Mtoto wake wa mwisho anaitwa Iyyana, amezaa na mpenzi wake mwingine, Mellisia Brim. Alishawahi kutumikia kifungo jela huko Las Vegas kwa kosa la unyanyasaji na vurugu.
       
Tangu mwaka 1996 ameshinda tuzo 30 bora zaidi duniani. Baba yake pia wa froyd alikuwa mpigaji na alipambana mapambano 35 akishinda 28 akipoteza


No comments:

Post a Comment