SHUJAA WA KEYSPORTS LEO TUNA MWANGAZIA MRISHO NGASSA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, January 17, 2019

SHUJAA WA KEYSPORTS LEO TUNA MWANGAZIA MRISHO NGASSA

Image result for mrisho ngasa


Imeandaliwa na Alex Mwenda...........watsap 0759-238235
MRISHO NGASSA
Shujaa wa keysports leo tunamwangazia mtanzania aliepata mafanikio makubwa katika soka la nchii hii ya Tanzania, kama ambavyo mwandishi wa makala hii Alex mwenda daady anamwangazia.
Jina lake ni Mrisho Ngassa (amezaliwa 5 Mei 1989) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Tanzaniaambaye anaichezea klabu mashuhuri Tanzania Young Africans FC 
Alianza maisha yake ya soka huko jijini mwanza katika timu za madaraja ya chini klaba ya kupandishwa kuichezea Toto afrikan wanakisha mapanda wa mwanza, kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa hakudumu klabuni hapo na kisha kutimkia mkoani kagera kwa timu ya kagera sugar wanankurukumbi mwaka 2005-2006.
Nakumbuka vizuri, Mrisho Ngassa alichomolewa kutoka mafichoni huko kwenye timu ya Geita Gold Mine na kocha aliyemfahamu siku nyingi, Sylvestre Marsh na kumpeleka Kagera Sugar timu aliyokuwa akiifundisha na kuipatia mafanikio, huko ndiko Ngassa alikoanza kujulikana.
Ngassa angeweza kuwa amejulikana kama angepata nafasi ya kucheza kwenye timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ iliyokuwa chini ya kocha Abdallah Kibadeni lakini hakubahatika kupata nafasi ya kucheza licha ya kuwemo kwenye timu hii, labda ilichangiwa na umbo lake lilivyokuwa dogo zaidi badala yake alianza kujulikana alipofanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara 2006 akiwa na Kagera Sugar ingawa mashindano yaliyomtoa yalikuwa ni yale ya Tusker mwaka 2006 yaliyofanyika Dar es Salaam hasa baada ya timu ya Kagera Sugar kuwafunga Simba 2-1 kwenye wa fainali.
Baada ya mashindano hayo Simba walikuwa wa kwanza kutangaza nia ya kumsajili Ngassa tena kwa kitita cha Sh 1 milioni lakini kwa mshangao wa wengi Ngassa aliwaita Yanga kwa kusema ‘Yanga njooni upesi kunisajili’ Yanga waliitikia wito na huo ukawa mwanzo wa Ngassa kutua Yanga.
Baada ya kutua Yanga, Ngassa alianza kuisaidia kupata mafanikio, baada ya kuukosa ubingwa wa Bara kupitia iliyoitwa ligi ndogo ya kubadili msimu mwaka huohuo mjini Morogoro, mwaka uliofuata Ngassa akisaidiana na wenzake waliipa Yanga ubingwa, huo ulikuwa mwanzo mzuri kwake kuwika Yanga na kuanza kuwa mchezaji tegemeo kwa muda wote huo licha ya kelele za wapenzi wa soka kutaka kocha wa Taifa Stars wakati huo, Marcio Maximo amwite kwenye timu ya Taifa, yeye alifumba macho akimtaka Ngassa aongeze bidii.
Haikuchukua muda mrefu, Maximo alimwita kwenye kikosi chake mwishoni mwa mwaka 2008, alifanikiwa kumbadilisha kiuchezaji kutoka kwenye ukimbiaji wa pembeni zaidi, hadi kucheza kwa malengo zaidi na akafanikiwa kumfanya kuwa mshambuliaji badala ya winga.
Msimu wa mwaka 2009 ulikuwa wa mafanikio zaidi kwa Ngassa, ambaye aling’ara vizuri akiwa na Yanga na timu za Taifa, hali hiyo ilimfanya kuanza kuutambua uwezo na mchango wake Yanga akilinganisha kipato chake (mshahara) mbele ya wachezaji wengi anaowazidi uwezo hasa wa nje kama Ben Mwalala, Jonh Njoroge na wengineo.
 Hatimaye aliamua kuanza mazungumzo na uongozi wa Yanga akiomba aboreshewe mkataba wake kwa kuongezewa mshahara, lakini uongozi chini ya Mwenyekiti Iman Madega ulipuuzia, hawakuuthamini mchango wake na ndipo Azam walipopata nafasi ya kufanya mazungumzo naye na kumsajili kuanzia msimu wa 2010/2011.
Hakuwa na msimu mzuri ndani ya Azam fc ambako nako walimtoa kwa mkopo kuelekea Simba sc mwaka 2012-2013 baada ya mkopo wake kumalizika alifanya maamuzi ya kurejea tena Yanga.
Kati ya mambo yanayonishangaza na hata kuwashangaza wachezaji wengi wa sasa na wale wa zamani ni jinsi Ngassa anavyojitofautisha na wachezaji wengine kwa kuonyesha mapenzi ya dhati Yanga, achilia mbali Ngassa kuibusu nembo ya jezi ya Yanga akiwa Azam na kuendelea kuwapungia mikono mashabiki wa Yanga alipokuwa Azam, Simba au akiwa Taifa Stars.
Mambo aliyojitofautisha na wachezaji wa zamani au hata wa leo ambao kwa nyakati tofauti wamezichezea Simba na Yanga kina Edibily Lunyamila, Mohammed Hussein, Ali Yussuf Tigana, Zamoyoni Mogella, Athumani China, Mwanamtwa Kihwelu, Omary Hussein, Godwin Aswile, Hamis Gaga, Method Mogela, Said Mwamba na wengineo hawakuwahi kuonyesha hadharani mapenzi ya dhati kwa timu waliyoipenda kama Ngassa.
Ilikuwa kawaida kwa Ngassa alipohamia Azam kumuona akiwa na bukta ya Yanga kabla ya kuvaa nguo za mazoezi za Azam, ni kawaida kwake kukaa katika upande wa mashabiki wa Yanga inapocheza michezo ya kimataifa au kirafiki na timu za nje siku ambayo Azam au Simba walikuwa mapumzikoni.
Hii inakuwa ni kielelezo cha mchezaji kuwa na mapenzi ya dhati kwa timu fulani hivyo sioni sababu ya timu nyingine kumuhangaikia.
Ngassa ni ‘Profesheno’
Ngassa amejitofautisha kimtazamo nje na ndani ya timu alizokuwa anazichezea za Azam na Simba, aliwahi kusema Kocha wa Simba Patrick Liewig kwamba ‘wachezaji wanapaswa kuiga uchezaji wa kujituma wa Ngassa ambaye aliijua na kuithamini kazi yake, alikuwa na nidhamu ya mazoezi na hata kambini.
Katika msimu wake wa kwanza tu akiwa Azam aliisaidia kushika nafasi ya tatu na yeye kuwa mfungaji bora msimu wa 2010/11 kwa mabao yake 16. Usingeweza kumtofautisha Ngassa wa Azam na Ngassa wa Yanga, tofauti ilikuwa ni majukumu na nafasi aliyopewa akiwa Azam hasa katika mfumo wa 4:3:3 iliomlazimu Ngassa kushambulia akitokea pembeni zaidi tofauti na alivyocheza Yanga, alikuwa akicheza kama mshambuliaji wa pili nyuma ya mshambuliaji wa kati kitu ambacho kilikuwa kinampa uhuru zaidi.
Angalau alipofika Simba na hasa baada ya Okwi kuondoka, Ngassa alipewa majukumu ya kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho, hali hiyo ilimfanya kuisaidia zaidi Simba, alikuwa chachu ya ushindi wa Simba, alitoa pasi nyingi za mwisho ambazo wachezaji wa Simba walizitumia kufunga.
Ni profesheno kwa sababu hakuonyesha kuchoka, alipigana sana ili timu yake ishinde, hakuonyesha mapenzi uwanjani kwani ni kati ya wachezaji ambao hawapendi kufungwa.
Ngassa aliushangaza umma wa Watanzania kwa kukataa kujiunga na El-Merreikh ya Sudan kwa sababu ya kutoshirikishwa katika mchakato mzima wa usajili, wadau wengi walimlaumu.
Binafsi nilimuunga mkono kutokwenda Sudan, si kwa sababu hakushirikishwa au sijui alifichwa na viongozi bali alikuwa sahihi kwa muono wa mbali.  Ligi ya Sudan ni maarufu kwao tu, kwa hiyo isingemsaidia Ngassa kutoka nje.

Baada ya kerejea kwa mara ya pili Yanga, Ngassa alitimkia Afrika kusini katika klabu ya Free states ambayo ilikuwa ikinolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi the flames Kinah Phili ambae alikuwa akimhusudu sana Mrisho Ngassa.

Hakudumu klabuni hapo baada ya kocha kinah phili kufungashiwa vilago nay eye kutimkia Fanja fc ya nchini Oman, ambako alidumu kwa mwezi mmoja na nusu klaba ya kuvunja mkataba na kurejea Tanzania. Jambo ambalo watu waliamini Ngassa analudi tena yanga lakini aliekuwa kocha wa wakati huo mholanzi Hans del pluijm alikataa kumsajiri na kasha aliamua kuachana na klabu hiyo.
Baada ya kuona dili lake la kutua Yanga limeshindikana alitimkia kwa wanakloma kumwantya Mbeya city ambako nako hakudumu kutokana na kudai stahiki zake na kasha kutimkia Ndanda fc ambako ndiko alifanikiwa kurejesha kiwango chake ambacho kilimfanya aweze kuludi tena yanga kwa mara ya tatu tangu mwaka 2006.

Ikumbukwe kuwa Mwezi wa Aprili 2009, Ngassa kutokana na uchezaji wake mzuri aliweza kumvutia aliekuwa kocha wa wakati huo wa west ham united  Francisco Zola klabu ya Uingereza kumualika ili aende kufanya majaribio ya wiki mbili nakumtizama uwezo wake wa kimpira ili waweze kumnunua, majaribio yalipoisha West Ham ilizungumzwa kua ni mchezaji mzuri ila anahitaji baadhi ya vitu fulani navyo ni vya kiufundi katika mambo ya kimpira hata hivyo inazungumzwa kua kuna baadhi ya klabu barani Ulaya zilipendelea kumchukua.

Mrisho Ngassa ndie mchezaji pekee nchini alietwaa mataji mengi zaidi ya ligi kuu Tanzania bara mara 7, kombe la tusker mara mbili.
Mrisho Ngassa alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu mwaka 2009-2010. Na mwaka huo huo alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu, adiidha alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa CECAFA CUP mwaka 2009, na tuzo kubwa kwake ni kuwa mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Afrika mwaka 2013-2014 kwa kufunga magoli 6.
Alichukua pia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wan ne msimu wa mwaka 2014-2015.
Mrisho Ngassa ndie mchezaji pekee wa Tanzania aliecheza mechi nyingi za timu ya taifa mara 100 huku akiwa ndie mfungaji bora wa muda wote ndani ya timu ya taifa ya Tanzania taifa stars akiwa na magoli 25.
Mrisho Ngassa amefunga ndoa na mrembo Ladhia Mngazija Tegeta mjini Dar es Salaam mwaka 2014. Hii ni ndoa ya pili kwa mchezaji huyo wa Yanga SC, ambaye alioa baada ya kuachana na mkewe wa awali.

Ngassa ndie mchezaji wa pekee kutoka Tanzania aliewahi kucheza dhidi ya Manchester united wakati akifanya majaribio ndani ya klabu ya Setter sounders ya marekani.
 Katika mchezo huoNgassa aliingia uwanjani kipindi cha pili katika dakika ya 76 na nusura awafunge mabingwahao katika dakika ya 89 baada ya kupiga shuti kali lililogonga mwamba. 

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa CenturyLink jijini Washington, Manchester ilifunga bao moja katika kipindi cha kwanza na mabao sita yakifungwa katika kipindi cha pili. 

Katika mabao hayo, matatu yakiwekwa kwenye kamba na Wayne Rooney aliyeingia kipindi cha pili huku Gabriel Obertan akikamilisha idadi ya mabao hayo dakika ya 89. 

Kipindi cha pili kilikuwa cha kasi huku kikiwa na sura mpya ambapo Manchester Unitedwalimuingiza Rooney huku Seattle Sounders wakibadili kipa Kasey Keller na kumuingiza 
Terry Boss. 

Ukiachana na Obertan na Rooney aliyefunga 'hat trick' katika dakika za 52, 69 na 72,wachezaji wengine waliofunga ambao katika mchezo huo ni Michael Owen (dk. 15), Mame Biram Diouf (dk. 49) na Ji-Sung Park (dk. 71). 

No comments:

Post a Comment