New
Na Alex Mwenda
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Ronald Koeman ni mzaliwa wa mji wa Zaandam
nchini Netherlands alizaliwa Tarehe 21 match 1963. Akiwa moja ya watu
waluozaliwa na kipaji chake Mguuni ronald Koeman alikuwa beki mahali wa kati au
kiungo mkabaji.
MAISHA YAKE YA SOKA
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Ronald Koeman alianza safari yake ya maisha ya
soka katika club ya Groningen mwaka mwaka 1980. Akiwa Club ya Groningen Koeman
ALicheza michezo 90 huku akifunga goli 33kuanzia mwaka 1980-1983 .
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Baada ya kuondoka Groningen Koeman alihamia
Club ya Ajax ambapo ALicheza michezo 94 na kufunga magoli 23 kuanzia mwaka
1983-1986. Akiwa Ajax Koeman alipata mafanikio makubwa baada ya kushinda kombe
ligi ambalo lilijukana kwa Jina la Eredevesie.
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
mwaka 1986 ronald Koeman alihamia Club ya psv
ambayo ni mahasimu wakubwa wa Ajax. Akiwa psv Koeman ALicheza michezo 98 na
kufunga magoli 51 ambapo alifanikiwa kushinda makombe matatu ya ligi mfululizo
kuanzia mwaka 1986 - 1989.
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
safari ya Ronaldo Koeman uliendelea ambapo
mwaka 1989 alijiunga na klabu ya Barcelona chininya Kocha Johan cryuff na
kuunda kikosi hatari kilichoitwa the dream team kuanzia mwaka 1989-1995.
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
akiwa Barcelona Koeman alifanikiwa kucheza
michezo 192 na kufunga magoli 67 ikiwa ni pamoja na kushinda kombe la Spain
alimaarufu kama la liga Mara nne mfululizo kuanzia mwaka 1991-1994, pia kwa
Mara kwake na club ya Barcelona ilishinda kombe la uefa champion League mwaka
1992 dhidi ya Sampdoria huku bao pekee likifungwa na Koeman kwenye uwanja wa
wembley.
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
baada ya kuondoka Barcelona ronald Koeman
alirejea nchini kwake na kujiunga na club ya feyenoord ambapo aliitumikia
kuanzia mwaka 1995-1997 akicheza michezo 61 na kufunga magoli 19
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
katika ngapi ya timu ya taifa ronald Koeman
alianza kuitumikia timu hiyo kuanzia mwaka1982-1997 akicheza michezo 78 na
kufunga magoli 14.akiwa na timu ya taifa ya Netherlands, Koeman alikuwa moja
kati mastaa wa timu hiyo iliyowajumuisha wachezaji nyota kibao wakiwemo Marco
van busten, Ruud Gullit, Frank Rijkaard na denis Bergkamp. Kikosi hiki atari
kijiti shares Sana miaka 1988, 1990 & 1994.
SIFA ZA RONALD KOEMAN
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Ronald Koeman alikuwa na sifa kibao zilizo
mfanya aonekani mchezaji bora kwa muda wake wote wa soka chache kati ya sifa
hizo ni :-
a) Koeman alikuwa ni mfungajiwa penalty mzuri
Sana.
b) Koeman alikuwa ni fundi wa kufunga magoli ya
free kick
c) Koeman alikuwa ni bingwa wa kufunga magoli
ya umbali mrefu kutokana na uwezo wake wa kupiga Mashuti makali golini.
d) ronald Koeman alikuwa fundi wa kupiga pasi
kwa umbali mrefu na mfupi pamoja na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
MICHEZO YAKE YOTE
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Katika maisha yake ya soka ronald Koeman
ALicheza michezo michezo 690 na kufunga magoli 239, pamoja na kushinda mataji
20. hapa nadiliki kusema kuwa Huyu Jamaa alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga
magoli.
MAISHA YA UKOCHA
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Baada ya kutundika daluga Koeman alianza maisha
mapya ya soka akiwa kama kocha. Katika maisha yake ya soka Koeman amefundisha
vilabu vingi Sana hadi Sana na kushinda mataji kadhaa.
a)akiwa kocha wa Ajax alifanikiwa kushinda
mataji matatu ya ligi mwaka 2001, 2002 & 2004.
b) baada ya kuachana na Ajax Koeman alihamia
PSV na kushinda mataji mawili ya ligi mwaka 2006&2007.
c) Baadae alivifundisha vilabu vya benifica ya
ureno, Valencia ya hispania, Southampton ya nchini England na sasa ni kocha wa
Everton ya nchini England pia.
TUZO BINAFSI ALIZOSHINDA
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Katika maisha yake ya soka, Koeman amefanikiwa
kunyakuwa tuzo nyingi Sana baadhi ya tuzo hizo
a) mchezaji bora wa Netherlands kwa miaka
miwili mfululizo 1987&1988.
b) Koeman alifanikiwa kuingia kwenye kikosi cha
uefa mwaka 1988
c) Koeman aliwai kuwa mfungaji bora kwenye
michuano ya uefa champion League kwa msimu wa mwaka 1993-1994.
akiwa benifica mwaka 2011-12 alishinda tuzo ya
Renus michels
pia akiwa akiwa nchini England amefanikiwa kuchukua
ya kocha bora wa Mwezi September 2014, January 2015, na January 2016.
RECORD ZAKE AMBAZO HAZIJAVUNJWA
![Description: https://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji117.png](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.png)
Katika safari yake ya soka akiwa kama mchezaji
ronald Koeman amefanikiwa kuvunja na kuweka record kadhaa. Chache kati ya
record zake ambazo mkapa sasa bado zinaisha ni :-
a) ronald Koeman ndie mchezaji wa Barcelona
anaeongoza kwa kufunga magoli mengi ya free kicks la liga akiwa amefunga magoli
25 akifutiwa na Leonel messi mwenye magoli 21 na Ronaldinho Gaucho mwenye
magoli 20. Moja kati ya record zilimshinda Leonel messi kuvunja katika Club ya
barcelona ni hii ya Huyu mwanaume wa shoka Koeman.
b) ronald Koeman anashikilia record ya kuwa
beki aliefunga magoli mengi Zaidi katika historia ya mpira wa miguu akiwa
amefunga magoli 239 katika mashindano yote.
HUYO NDIE RONALD KOEMAN KOCHA WA SASA WA timu
ya taifa ya uholanzi.
No comments:
Post a Comment