Na Alex Mwenda
Kuna waamuzi
wengi ambao wamefanikiwa katika maisha ya uchezeshaji wa mpira wa miguu na
kufanikiwa kutengenezaa majina katika ulimwengu huu wa soka na kujitengenezea
umaarufu mkubwa pamoja na kuingiza pesa nyingi sana.
Hii leo
ukizungumzia waamuzi maarufu duniani utasema Michael Oliver, Antony Tyler na
waamuzi wengine wengi zaidi.
Hapa nchini
Tanzania waamuzi waliopata umaarufu ni wengi akiwemo Israel Mujuni Nkongo,
Joseph Mapunda, Herry Sasi, Hans mabena na wengine wengi.
Kazi ya
uamuzi ni yenye lawama na ubabaishi mtupu kwa wale wasiojua kutafsiri sheria
kumi na saba za mchezo wa soka, mwamuzi Jonas
Eriksson kutoka sweeden ndie mwamuzi milionea zaidi duniani, na kuna
wengine wameshindwa kutafsiri sheria 17za mchezo wa soka na kushuhswa hadhi
zao.
Keysports
ndani ya shujaawetu tuna mwangazia mwaamuzi wa kike alieleta mapinduzi makubwa
katika ngazi hii ya uamuzi wa mpira wa miguu nchini, Jonesia Rukya.
Jina lake
halisi ni Jonesia Rukya Kabakama alizaliwa mkoani Kagera Kaskazini magharibi
mwa Tanzania, ambapo alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi na sekondari
mkoani humo.
Mwaka 2006
Jonesia Rukya alianza rasmi kujihusisha na masuala ya mchezo wa soka akiwa kama
mchezaji katika timu ya hukohuko mkoani Kagera.
Baada ya
kuona hakuna mafanikio yoyote aliamua kuacha na kuanza kujifunza masuala ya
uamuzi jamba ambalo lilimtenganisha na sehemu kubwa ya familiaa yake kutokana
na familia yake kutopenda anachokifanya.
Hakukata
tamaa na mtu pekee aliekuwa akimsaidia na kumsapoti ni bibi yake jambo ambalo
liliendelea kumtia nguvu kutokana na mchezo huu kuwa ndani ya damu yake.
Tangu mwaka
2006 alichezesha mechi za madaraja ya chini mpaka mwaka 2011 ambapo aliinuliwa
na kupandishwa kuchezesha ligi daraja la kwanza mechi kati ya Rhino rangers vs
AFC mchezo uliopigwa mkoani Arusha.
Rasmi mwaka
2014 alichaguliwa kuchezesha mechi ya Mtani jembe kati ya Yanga vs Simba, kitu
ambacho kilimpa umaarufu na kujiamini zaidi na hapo ndipo fursa zingine
zilifunguliwa kwa mwanamama huyu mashughuri zaidi barani Afrika na ulimwenguni
kwote.
Alisimama
pia katika derby ya Simba na Yanga September 30 mwaka jana katika mchezo
ulipigwa uwanja wa taifa na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Jonesia
Rukya kabla ya kuwa mwamuzi nchini Tanzania, alikuwa mwalimu na mjasiliamali na
aliweza kumudu vitu vyote viwili kwa wakati mmoja japo ilikuwa ni changamoto
kubwa kwake.
Jonesia
amepata nafasi ya kuchezesha michuano mikubwa AFrika ya kinamama, mwaka 2017
alichezesha michuano ya AFCON ya kina mama nchoni Cameroon, na mwaka 2018
alikuwepo pia nchini Ghana katika michuano hiyo.
Alichezesha
michezo miwili, Mali na Cameroon hatua na makundi pamoja na Afrika kusini na
Mali hatua ya nusu fainali.
Jonesia
Rukya pia ni miongoni mwa waamuzi wachache watakaochezesha michuano ya kombe la
dunia kwa wanawake mwaka huu nchini Ureno.
No comments:
Post a Comment