Mohamed Salah pikipiki isiyo kamatika kwa urahisi - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, January 10, 2019

Mohamed Salah pikipiki isiyo kamatika kwa urahisi


Image result for mo salah wife age
Na Alex Mwenda
Misri imewahi kuwa na kizazi cha dhahabu, kizazi ambacho kilikuwa na
kila aina ya nyota ndani ya kikosi chao.
Kikosi ambacho ndani ya miongo mitatu kilifanikiwa kushinda kombe la
Mataifa huru ya Afrika (Afcon) Mara nne. ( 1998, 2006,2008, na 2010).
Kikosi hiki kilikuwa chini ya kocha Hassan Sheheta, kocha ambaye
aliipa mafanikio makubwa nchi yake ya Misri.
Alitengeneza kikosi imara ambacho kinasemekana ndicho kilikuwa kizazi
cha dhahabu.
Kizazi ambacho kiliwafanya Wamisri waone kushinda kombe la mataifa
huru ya Afrika (Afcon) kwao ni kitu cha kawaida.
Wengi walikinai ƙikombe hiki wakabaki na kiu moja tu nayo kwenda
kombe la dunia. Mara ya mwisho kwa Misri kushiriki kombe la dunia ilikuwa mwaka 1990.
Hivyo kila mtu katika miji ya Cairo, Alexandria na miji mingine ya
Misri alikuwa na shauku kubwa ya kuishuhudia timu yao ikiwa inacheza
kombe la dunia.
Imani ya Wamisiri ilikuwa kubwa sana juu ya kikosi cha Shehata kwa
sababu waliamini kikosi kile kilikuwa kinauwezo wa kuwapeleka kombe la
dunia.
Utamwambia nini Mmisri juu ya Mohamed Aboutrika akuelewe?
Kiungo ambaye kwao wao wanaamini ndiye kiungo bora kuwahi kutokea
katika kizazi cha soka barani Afrika.
Kiungo ambaye alikuwa na uwezo wa kuibeba timu mabegani mwake na kukimbia nayo.
Vipi kuhusu kipaji cha Mohamed Zidan? Kipaji ambacho kilikuwa
kinafurahisha kwa kiasi kikubwa kukitazama machoni kwa sababu ya uwezo
wake mkubwa wa kucheza mpira.
Kizazi hiki kilipita, kiliweka alama kubwa kwenye historia ya mpira wa
miguu duniani. Alama ambayo ni vigumu kufutika.
Alama ambayo itabaki kwenye kumbukumbu ya Wamisri wengi, lakini kikosi
hiki hakikukidhi matarajio ya Wamisri.
Image result for mo salah wife age
Matamanio yao makubwa yalikuwa ni wao kushiriki kombe la dunia.
Walitamani kushindana na timu bora zaidi ya timu za Afrika ambapo wao
waliona imetosha kwao kuwa wababe wa Afcon , hivo walitamani kwenda
sehemu kubwa zaidi ya hiyo.
Sehemu ambayo kila jicho la dunia litashawishi ubongo kuwapigia makofi
na kukiri kwa vinywa kuwa Misri imebarikiwa kuwa na vipaji.
Lakini cha kusikitisha zaidi kikosi kile bora cha dhahabu cha kina
Shehata kilishindwa kufikia matamanio ya Wamisri.
Kilipita kizazi kile huku kikiwaacha Wamisri katika huzuni kubwa sana
ambayo ilikosa mtu wa kuja kuwafariji kwenye huzuni hiyo.
Miaka 28 imepita, miaka ya mateso na huzuni kubwa. Miaka ambayo
Wamisri walitumia muda mwingi kuwaangalia wenzao kwenye luninga
wakipambana katika kombe la dunia.
Lakini baada ya miaka 28 ametokea mfariji wao, mfariji ambaye
ametimiza matamanio yao ya siku nyingi. Matamanio ya kushuhudia kombe
la dunia huku timu yao ikiwa ndani ya mashindano.
Kikosi kilichokuja kuwafariji ni tofaufi na kikosi ambacho walikuwa
wanakitegemea siku zote.
Wamekuja kufarijiwa na watu ambao kwa asilimia kubwa hawapo kwenye
mnyonyoro wa kikosi kile cha dhahabu.
Leo hii kina Mohamed Elneny ndiyo mashujaa wapya na wakubwa katika
ardhi ya Misri.
Leo hii historia ya soka la Misri itamtazama kwa ukubwa Mohamed Salah
juu ya kina Aboutreka.
Mohamed Salah amekamilisha furaha yao ambayo ilikuwa haijakamilika.
Kila mtu alisubiri kwa hamu ikamilike.
Lakini alikosekana mtu sahihi wa kuikamilisha ile furaha, lakini Salah
ndiye ambaye amekuja kukikamilisha.
Vilio vya furaha vilitawala katika nchi ya Misri, kila sehemu watu
wengi walitembea kuonesha furaha yao kwa matokeo hayo.

MSHAMBULIAJI matata wa Ligi kuu ya Uingereza (EPL) akiwakilisha Liverpool, Mohamed Salah wa Misri alizaliwa Juni 15, 1992, kipindi Kenya ikijipa demokrasia ya vyama vingi vya kisiasa.

Alizaliwa katika mtaa wa Gharbia huko Misri na tangu utotoni, soka imekuwa kama ndugu yake wa toka nitoke.
Alianza usakataji wake wa kabumbu katika Klabu ya El Mokawloon na 2010 akawa ametambulika kama sogora matata na akaingia katika timu ya taifa.

Mwaka wa 2012 aliingia katika safu ya kulipwa nchini Uswizi ambapo alisajiliwa na Klabu ya FC Basel. Alisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uswizi katika msimu wa 2012/13 na kisha akaisaidia kutwaa Kombe la Uhren mwaka uo huo wa 2013.

Januari 2014 aliingia katika klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza na akawa mchezaji wa  wa kwanza kabisa wa uraia wake kuwahi kuichezea Chelsea.

Alisajiliwa kwa mkopo na Klabu za Roma na Fiorentina huku Chelsea ikiwa na ubutu wa kutambua uwezo wa Salah na ndipo akiwa katika mahangaiko ya mikopo hiyo, Liverpool ikamtambua na ikamsajili.

Mwaka wa 2017 ambao ndio mwaka Liverpool ilimnasa, alitangazwa na Shirikisho la kandanda barani Afrika na pia Shirika la habari la Uingereza (BBC) kama mchezaji bora wa mwaka.

Amekiri kuwa kimasomo alikuwa hajielewi kabisa na kuwa wakati hakuwa akicheza mpira ujanani wake, alikuwa akitazama mchuano wa mpira.
Alimaliza msimu wa 2017/18 akiwa kidedea kwa kutinga magoli 36.

Mohamed Salah ametwaa tuzo nyingi kwa mwaka 2018, ikiwemo mfungaji bora wa ligi kuu nchini England, mchezaji bora wa msimu uliopita nchini England, mchezaji bora wa Liverpool,mchezaji bora wa kigeni, mchezaji bora wa chama cha waandishi wa habari za michezo England, alishika nafasi ya tatu katika tuzo za mchezaji bora wa dunia, mchezaji bora wa BBC, mchezaji bora wa Afrika, mchezaji bora wa Misri.

Mohamed Salah ndie mchezaji pekee alietwaa tuzo nyingi kuliko yeyote duniani kwa mwaka 2018. Hapo sio Messi wala Ronaldo hata Modric ambao wamefua dafu mbele yake.

Ana umri wa miaka 26 sasa, ameichezea Liverpool mechi 57 na kufunga mabao 45, huku akiitumikia Misri katika mechi 62 na kufunga magoli 39. Mohamed Salah amemwoa Bi Maggie mwaka 2013 ambae walisoma pamoja shule, na kufanikiwa kupata mtoto mmoja aitwae Maccer aliezaliwa mwaka 2014.




No comments:

Post a Comment