MTIBWA SUGAR YATOA TUZO KWA WALIOFANYA VYEMA MSIMU ULIOPITA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, July 9, 2018

MTIBWA SUGAR YATOA TUZO KWA WALIOFANYA VYEMA MSIMU ULIOPITA


Timu ya Mtibwa Sugar Sports Club jana ilifanya hafla ya kuwapongeza wachezaji wa kikosi hicho kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu 2017/2018, hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya New Africa Hotel ya jijini Dar es salaam.
Hafla hiyo ilianza saa 1:00 usiku katika hoteli ya New Africa Hoteli, tuzo ya kwanza katika hafla hiyo kutolewa ilikuwa tuzo ya goli bora la msimu timu ya vijana  iliyokwenda kwa Richard William Mwamba dhidi Stand United katika fainali ya Uhai aliekuwa anawania na Abuu Juma Salum na Abdul Yusph Haule.
Tuzo ya pili ilienda kwa Aboutwalib Mshery aliyechaguliwa kipa bora wa timu ya vijana aliyekuwa anashindana na Aden Salvatory Luhavya.
Kibwana Ally Shomary alibeba tuzo ya mchezaji aliyecheza dakika nyingi kwa timu ya viajana, na tuzo ya nne ilienda kwa Abuu Salum Juma baada ya kuwabwaga Kibwana Ally Shomary, Richard William Mwamba na Onesmo Justin Mayaya kwa mchezaji mwenye aliyechaguliwa na mashabiki kwa upande wa timu ya vijana.
Tuzo ya tano ilienda kwa mchezaji mwenye nidhamu bora katika timu ya vijana na mshindi alikuwa Dickson Nickson Job  ambaye alikuwa anashindana na Kibwana Shomary na Jamal Idd Masenga.
Tuzo ya mchezaji bora wa timu ya vijana ilienda kwa Onesmo Justin Mayaya ,wengine ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo ni Dickson Nickson Job, Abuu Salum Juma.
Tuzo ya mwisho kwa timu ya vijana ilienda kwa kocha wao Vicent Barnabas Salamba kwa niaba ya benchi la ufundi la timu ya vijana.
Kwa upande wa timu kubwa goli bora la msimu lilienda kwa Salum Kihimbwa dhidi ya Singida United katika fainali ya kombe la shirikisho, wengine waliokuwa wanawania tuzo hiyo ni  Ally Makarani dhidi ya Buseresere, Kelvin Sabato dhidi ya Azam, Issa Rashid dhidi ya Singida United katika fainali ya kombe la shirikisho na mwisho ni Ismail Aidan Mhesa dhidi ya Singida United.
Salum Kihimbwa aliendelea kungara katika tuzo hiyo baada ya kunyakua tuzo ya pili ya mchezaji bora anayechipukia na tuzo hii ilikuwa tuzo ya pili katika usiku huo wa tuzo baada ya kuwashinda Ally Makarani na Ismail Mhesa.
Benedicto Tinocco alinyakua tuzo ya kipa bora wa msimu kwa usiku wa jana, tuzo hiyo alikuwa anapata upinzani mkubwa kutoka kwa Shabani Kado na Abdallah Makangana.
Hassan Suleyman Isihaka beki kitasa kutoka kwa wana tam tam yeye aliibuka na tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu bora kwa timu ya wakubwa, wengine ambao walikuwa wania tuzo hiyo ni Shabani Mussa Nditi na Dickson Daud.
Dicskon Daud Mbeikya yeye alibeba tuzo ya mchezaji aliyecheza dakika nyingi na tuzo hiyo haikuwa na mpinzani kutokana na kucheza dakika 2700 katika ligi kuu bara (Vodacom Premier League) na kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup).
Shaban Mussa Nditi yeye alibeba tuzo ya mchezaji bora mwandamizi katika usiku huo, Nditi alipata upinzani kutoka kwa Henry Joseph Shindika na Dicskon Daud Mbeikya.
Pichani: Shabani Mussa Nditi akiwa ameshikilia tuzo yake pamoja na Issa Kajia 
Mfungaji bora wa msimu alikuwa ni Hassan Dilunga baada ya kufunga magoli 9 katika msimu huu , huku ligi kuu bara akifunga goli 5 na goli 4 kombe la Azam Sports Federation Cup.
Dilunga aliendelea kungara baada ya kuchaguliwa kama mchezaji bora wa msimu na kufikisha tuzo ya pili katika usiku wa jana,wengine waliokuwa wanawania  tuzo hiyo ni Shabani Mussa Nditi, Cassian Ponera, Dickson Daud Mbeikya na Salum Kihimbwa.
Tuzo ya 16 katika usiku wa jana na tuzo ya mwisho ilienda kwa benchi la ufundi Zuber Katwila na Patrick Mwangata ambao walipewa tuzo kutokana kuiongoza timu kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho na timu yenye nidhamu bora katika ligi kuu bara.
Pichani: Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Estates Limited  Seif A. Seif akimkabidhi Zuber Katwila tuzo 
 

No comments:

Post a Comment