Michuano ya
kombe la dunia ilianza kutimua vumbi mnamo miaka ya 1930 huko nchini Uruguay na
kuwashuhudia wenyeji wakilitwaa kombe hilo lakini wakarudia tena 1950 kwa
kulitwaa tena na ndo ilikuwa mara yao ya mwisho kuweka makwapani taji hilo
kubwa katika mchezo wa soka.
Mwaka 2018
Russia ndio wameandaa kombe la dunia na kushudia mengi ya kitokea kuondolewa kwa
Messi na Argentina yake kadharika Ronaldo na Ureno yake bila kusahau Neymar na
Brazil yake.
Keysports
inawakumbusha kuwa hizo habari za kutolewa kwa mastaa wakubwa hazina utamu sana
kama kuelekea mechi ya nusu fainali ya kwanza kati ya Ufaransa na Ubelgiji
unajua nani atasonga au nani atamtambia mwenzake??
Picha ya
hawa watu ilianza mnamo mwaka 1904 ambapo timu hizi zilitoka sare ya mabao 3-3
pale nchini Ubelgiji ilikuwa ni siku ya wafanyakazi namaanisha tarehe 1.5.1904
Hizi timu
hazina uhasama bali ni marafiki wakubwa sana tangu urafiki wao ulipoanza mnamo
mwaka 1904. Baada ya ile namjua namjua na matokeo kwenda sare wakaomba tena
mechi ya kirafiki ili urafiki wao uzidi kudumu mwaka huo huo Ufaransa
walinogewa na mchezo mtamu wa wapinzani wao Ubelgiji kutokana na utamu wa mabao
3-3.
Ubelgiji
walikubali ombi lao na kurudia mechi, sio kwa Afrika tuu tamaduni hii ya
kunogewa na mchezo na matokeo kumbe ilikuwepo pia miaka hiyo. Nakumbuka pia
timu za magagura, lusonga na hata litisha na magima minogo ilikuwa sana wakati
ambao Alex Mwenda Daady anatamba kwelikweli na yimu mbalimbali ikiwepo Masangu
fc ya huko Magagura.
Tarehe
7.5.1904 walishuka dimbani tena na Ubelgiji kushinda mabao 7-0 hapo ndio
Ufaransa walipoamka kisoka na kuamini kumbe watakiwa kuwa serious uwanjani,
walirejea makwao kwa hudhuni kubwa sana na kaahidi kuwa undugu wao utaendelea
na mwaka 1906 Ufaransa waliwaarika ubelgiji na wakiwa nyumbani waliduwazwa kwa
bao 5-0.
Hapo ndipo
Ufaransa waliona kuwa hapana undugu ndani ya dakika 90 watu wapo makini sana
mwaka 1907 Ufaransa walishuka tena dimbani dhidi ya ubelgiji nchini ubelgiji na
Ufaransa kushinda kwa magoli 2-1..Unaweza kusema kuwa Ubelgiji waliamua
kuwaachia tuu Ufaransa maana mpaka dakika za mwishoni mwa mchezo walikuwa nyuma
kwa goli 1-0.
Hizi timu
mbili zimekutana mara 73 tangu mwaka 1904, na Ubelgiji wao wakishinda mara 30
kwenda sare mara 19, huku Ufaransa wao wakishinda mara 24.
Kwa mara
zote Ubelgiji ndie anaeshikiria rekodi ya kumfunga Ufaransa magoli mengi
zaidi mwaka 1905 ushindi wa mabao 7-0
lakini wakairudia tena rekodi hiyo mwaka 1911 wakishinda ubelgiji kwa goli 7-1.
Ubelgiji
waliifunga pia Ufaransa magoli 6-1, na Ufaransa wao wameshikiria rekodi ya
kuifunga ubelgiji mabao 5-3 mwaka 1938.
Rekodi
zinaonesha katika michuano ya kombe la dunia timu hizi zimekutana mara 5 na
Ufaransa wakishinda mara 3, sare mara moja na ubelgiji wakishinda mara 1 pekee.
Taswira hii
inaonesha kuwa Ufaransa nafasi ya kutinga fainali ni kubwa kuliko Ubelgiji japo
wataalamu wa masuala ya utabiri nao wakiipa Ufaransa nafasi ya kushinda kwa 39%
droo 30% na ubelgiji 31%
Mara ya
mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni mwaka 2015 tarehe 7/6 ambapo Ubelgiji
waliitambia Ufaransa kwa magoli 4-3.
Berther
Conte ni shabiki mkubwa sana wa Killian mbape Rotin hana utofauti na Salama Idd
Maridadi lakini nawaambia nusu fainali hii tuheshimiane kwanza.
Huku Lukaku,
hapa Griezman, pale Hazard kule Mbape Lotini, hatoki mtuuuu hapa Rloris hapa
Courtious.
Makala hii
imeandaliwa na Alex Mwenda ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha michezo kutoka
KEYFM SONGEA pia mtangazaji wa mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment