YANGA YAMPA NYONI UFALME HUU SIMBA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, May 2, 2018

YANGA YAMPA NYONI UFALME HUU SIMBA

Achana na bao alilolifunga dhidi ya Yanga, Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amemtangaza beki wake kiraka Erasto Nyoni kuwa ndiye mchezaji wake bora kikosini mwake.

Nyoni katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga, alifunga bao pekee lililoipa ushindi Simba wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Beki huyo mkongwe hivi sasa ni tegemeo katika kikosi cha Simba ambacho amejiunga nacho msimu huu akitokea Azam FC am­bako alimaliza mkataba wake.

Lechan­tre alisema ana kila saba­bu ya kumwagia sifa Nyoni kutokana na mchango mkubwa anaoutoa katika timu yake inayoongoza ligi ikiwa na pointi 62.

Lechantre alisema, beki huyo anatimiza vizuri majukumu yake katika ku­zuia na kupunguza hatari langoni, hivyo anastaili sifa za kuwa mchezaji bora na beki bora wa timu yake.

“Nyoni amekuwa katika kikosi cha kwanza cha timu yangu kutokana na jinsi anavyoweza kutimiza majukumu yake, ni ngumu kwangu kumuweka nje.

“Wachezaji wa aina ya Nyoni ndiyo ninaowahitaji katika timu yangu na hata ukiniuliza mchezaji gani bora wa mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga nitamtaja yeye tofauti na bao lake alilolif­unga.

“Nyoni ndiye anayeion­goza safu ya ulinzi vizuri kwa kuwapanga mabeki wenzake na kuwakum­busha majukumu yao,” alisema Lechantre.

No comments:

Post a Comment