Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, amekula shavu la ubalozi kutoka Kampuni ya Star Times wa michuno ya Kombe la Dunia inayotarajia kuanza nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu.
Ajibu amekuwa miongoni mwa Mabalozi watakokuwa wanawakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo kupitia Star Times.
Mwingizaji Wema Sepetu naye amekuwa miongoni mwa Mabalozi wanaohusika na Kampuni hiyo itakayoonesha mechi zote za Kombe la Dunia mwezi June.
Hafla ya kuwatangaza Mabalozi hao imefanyika leo katika Ukumbi wa SlipWay, Masaki, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment