Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, amekuwa miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kuwa Mabalozi wa michuano ya Kombe la Dunia chini ya Star Times inayotaraji kuanza mwezi Juni mwaka huu nchini Russia.
Mkude ameungana na Ibrahim Ajibu wa Yanga ambaye ameteuliwa pia kuwa mmoja wa Mabalozi kuelekea mashindano hayo kuanza.
Star Times watakuwa wanaonesha mechi zote za michuano hiyo kupitia king'amuzi chao kuanzia Juni 2018.
Michuano hiyo kwa mwaka huu itafanyika nchini Russia baada ya miaka minne iliyopita kufanyikia Brazil.
No comments:
Post a Comment