WANALIZOMBE WA MAJIMAJI KUJIPIMA UBAVU HAPO KESHO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, May 2, 2018

WANALIZOMBE WA MAJIMAJI KUJIPIMA UBAVU HAPO KESHO

Image result for majimaji fc
...Picha mchezaji wa Majimaji Paul Mahona akijaribu kumdhibiti vilivyo mshambuliaji wa klabu ya Simba Emmanel Okwi (kulia)

Na Alex Mwenda Daady-Songea
Klabu ya Majimaji ya mjini Songea inatarajia kushuka dimbani hapo kesho siku ya alhamisi katika uwanja wa majimaji kumenyana na mabingwa wa mkoa wa Ruvuma, timu ya Black Belt Fc mechi inayotarajia kuwa ya upinzani wa hali ya juu sana kutokana na timu hizi kufahamiana vilivyo.

Majimaji wanatarajia kuutumia mchezo huo kama maandalizi ya mechi yao ya tarehe 6 mwezi huu dhidi ya Mtibwa sugar mchezo ambao utapigwa katika dimba la majimaji.

Aidha Black Balt wao wanatarajia kuutumia mchezo huu ikiwa ni maandalizi ya mechi zake za mabingwa wa kanda ambapo wamepangwa kundi B mkoani Rukwa pamoja na timu za  Laela FC ya Rukwa, Tukuyu Stars ya Mbeya, Tabora FC ya Tabora, Migombani FC ya Songwe, Kasulu Red Star FC ya Kigoma, Black Belt ya Ruvuma na Watu FC ya Katavi.

Hiyo inatarijia kuanza kutimua vumbi hapo Jumapili.

No comments:

Post a Comment