MICHEZO Rufaa ya Young Africans yawekwa kapuni - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, May 3, 2018

MICHEZO Rufaa ya Young Africans yawekwa kapuni

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) imekataa malalamiko ya Yanga kutaka ipatiwe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu dhidi ya Mbeya City kwa timu hiyo kuwa na mchezaji zaidi kwenye mechi, kwa vile hakuna Kanuni yoyote ya Ligi Kuu inayoweza kubadili matokeo ya uwanjani kwa mazingira hayo.
 
Kwa mujibu wa uamuzi huo, hakuna namna yoyote ile mchezaji anayezidi (extra player) kubadili matokeo ya mchezo.

Aidha, kwa mujibu wa kanuni, katika mazingira ambayo mchezaji aliyezidi akiwa uwanjani na likafungwa goli, mwamuzi atalikataa.

Hivyo, kutokana na kanuni za Ligi kutojitosheleza katika suala hilo la extra player, Kamati hiyo imeeleza kuwa iliangalia Kanuni za FIFA kwa umakini kabla ya kufikia uamuzi huo.
Mchezaji Ramadhan Malima wa Mbeya City ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini akatoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwenda kushangilia bao la kusawazisha la timu yake amesimamishwa hadi suala lake litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Kamati imeeleza kuwa uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.
Kwa upande wa waamuzi, imeelezwa kuwa kulikuwa na upungufu katika suala la kusimamia ubadilishaji wa wachezaji (substitution), hivyo Kamati ya Waamuzi ya TFF imeandikiwa barua ili ichukua hatua dhidi ya wahusika. 

No comments:

Post a Comment