MARTIAL KUTIMKIA CHELSEA, TETESI KIBAO ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, May 2, 2018

MARTIAL KUTIMKIA CHELSEA, TETESI KIBAO ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO

Naibu mkufunzi wa Liverpool Zeljko Buvac anapigiwa upatu kumrithi mkufunzi wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger . (Pravda BL, via Mirror)
Arsenal huenda isimlipe mkufunzi wake mpya zaidi ya kitita cha £8.5m ambacho mkufunzi wake Arsene Wenger alikuwa akipata kwa mwaka (Daily Mail)
Beki wa Manchester United Eric Bailly, 24, ana wasiwasi kuhusu hatma yake katika klabu hiyo baada ya kutochezeshwa na mkufunzi wa klabu hiyo Jose Mourinho. (Mirror)
Mabeki Matteo Darmian na Daley Blind, wote wakiwa na umri wa 28 wameambiwa kwamba wako huru kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Times)
Chelsea inamnyatia Anthony Martial, 22, iwapo Manchester United haiwezi kumrai raia huyo wa Ufaransa kusalia katika klabu hiyo ya Old Trafford (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Roma Radja Nainggolan, 29, amepinga madai kwamba anahusishwa na uhamisho wa Chelsea na Manchester United kwa kuamua kusalia katika klabu hiyo ya Serie A. (Daily Mail)
Huenda wakufunzi wa Chelsea na Napoli Antonio Conte na Maurizio Sarri wakabadilishana vilabu.(mirror)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho amethibitisha kwamba kumekuwa na hamu ya mchezaji huyo kutoka nje huku klabu za Manchester United na Manchester City . (Manchester Evening News)

No comments:

Post a Comment