KAMATA ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI MASTAA AMBAO KANDARASI ZAO ZIMEFIKA UKINGONI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, May 3, 2018

KAMATA ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI MASTAA AMBAO KANDARASI ZAO ZIMEFIKA UKINGONI

Dirisha la uhamisho la ligi ya Uingereza halifunguliwa hadi 17 Mei lakini kuna wachezaji wengi waliokamilisha kandarsi zao ambao wako tayari kufunga virago na kuondoka.
Miongoni mwao ni kiungo wa kati wa Arsenal
Jack Wilshere, ambaye amepewa mkataba mpya Arsenal, wachezaji wawili wa Bayern Arjen Robben na Franck Ribery na kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can.
Lakini je unawajua wachezaji wngi ambao walionyesha mchezo mzuri msimu huu kulingana na shirika la utafiti la soka CIES footbal Observerytory?
Kundi hilo la utafiti limetengeza orodha ya wachezaji 50 kulingana na majukumu sita ya wachezaji ikiwemo, kupokonya mpira, kusambaza, kutengeza na fasi za magoli, kushambulia. Kipa wanapimwa kulingana na mbao waliofungwa kwa dakika mbali na asilimia ya mabao waliookoa.T
Wachezaji 10 ambao wamekamilisha kandarasi zao
Shirika hilo la utafiti wa soka CIES linawapima wachezaji hao katika viwango vya hadi 100 kutoka wale waliocheza hadi chini ya dakika 10000 msimu huu. Orodha hiyo ya kumi bora inawapigia upatu mabeki kutoka Itali , iwapo kocha wa Liverpool anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi.
1. Pepe Reina – ameorodheshwa wa 91. Kipa huyo mwnye umri wa miaka 35 aliyeichezea Liverpool ameisaidia Napoli kusalia katika ligi ya Serie A akiwa hajafungwa kwa takriban mechi 17 ikiwa ni zaidi ya kipa yoyote yule.
2. Vicente Guaita – ameorodheshwa wa 90. Kipa huyo wa Getafe, 31, imeripotiwa alitia kandarasi na Crystal Palace mapema msimu huu lakini sasa amepokea maombi kutoka Atletico Madrid. Raia huyo wa Uhispania ana rekodi nzuri ya kuokoa mashambulizi.
3. Nafasi ya tatu. Arjen Robben – ameorodheshwa wa 89. Winga huyo wa Bayern mwenye umri wa miaka 34 huenda amepunguza kasi yake lakini kwa kuwa ni mchezaji anayeweza kutamba na mpira anaweza kuwa na thamani nzuri. Tayari amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kusalia na klabu hiyo.
3..Nafasi ya 3. Gianluigi Buffon – ameorodheshwa wa 89. kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 ameonyesha ubora wake Juventus msimu huu. Anatarajiwa kustaafu mwisho wa msimu huu ijapokuwa amesema kuwa huenda akaendelea.
5. Andrea Barzagli – Ameorodheshwa wa 86. Ana sifa za kuimarisha safu ya ulinzi ya Juventus akishirikiana na Giorgio Chiellini, baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya 21 msimu huu. Kumuuza mchezaji huyo wa umri wa miaka 36 nje ya Juventus itakuwa vigumu.
6. Andrea Masiello – Ameorodheshwa wa 84. beki huyo wa klabu ya Atalanta 32, amekuwa katika ligi ya Serie A tangu kashfa ya kuuza mechi 2011 lakini ameonyesha thamani yake msimu huu huku klabu hiyo ikiwa na lengo la kufuzu katika michuano ya ligi ya Yuropa.
6. Emre Can – Ameorodheshwa wa 84. Amehusishwa pakubwa na uhamisho wa Juventus, iwapo mchezaji huyo wa kiungo cha kati atafanikiwa kuvutia mchezaji mmoja wa Turin kujiunga na Liverpool .Ana mabao matatu katika ligi ya premia na ametoa pasi 4 zilizosababisha magoli katika msimu wa 2017-18,.
8. Milan Badelj – Ameorodheshwa wa 83. mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ametoa pasi nzuri katika kila mechi ikilinganishwa na mchezaji mwengine yeyote wa klabu ya Florentina msimu huu huku ikiripotiwa kwamba Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia raia huyo wa Croatia.
8. Kwadwo Asamoah – ameorodheshwa wa 83. Inter Milan wanapigiwa upatu kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia anaweza kucheza katika kiungo cha kati. Mchezaji huyo wa Ghana pia anahusishwa na uhamisho wa Everton na Tottenham.
8. Rafinha – ameorodheshwa katika nafasi ya 83. Mchezaji huyo wa Bayern mwenye umri wa miaka 32 amepewa kandarasi mpya ya kusalia na mabingwa hao wa Bundesliga lakini hakupendelea.
Majina ya wachezaji nyota ambao bado wana thamani
Chini katika orodha kuna wachezaji ambao wanaonyesha umahiri wao na ambao bado wanaweza kuwa nyota wa Ulaya.
11. Franck Ribery – Ameorodheshwa wa 82. Kama Robben, winga huyo wa Ufaransa amepewa mkataba mpya wa kusalia Bayern ambapo anaweza kushinda taji lake la tisa la Busliga lakini huenda akeleka katika klabu nyangine kw amkataba wa kudumu ughaibuni
13. Jack Wilshere – Ameorodheshwa wa 81. Kuimarika kwa kiungo huya wa kati wa Arsenal ambako kumezongwa na majeraha lakini ni mchezaji ambaye amekuwa akitamba na mpira zaidi ya kiungo wa kati mwengine yeyote katika ligi ya Uingereza. Je kupunguzwa kwa mshahara wake kutamfanya asalie katika klabu hiyo?
18. Sergio Canales – ameorodheshwa wa 78. Klabu ya Real Betis ni miongoni mwa klabu ambazo zimeripoti kuwa na hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Real Sociedad ambaye ametoa pasi 11 zilizosababisha mabao katika mashindano yote msimu huu.
18. Stefan de Vrij – Ameorodheshwa wa 78. beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26 ameshiriki katika mechi za Lazio msimu huu, akifunga mabao mengi zaidi ya beki mwengine yeyote wa Serie A.
Raia huyo wa Uhalonzi amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan, Manchester United na Barcelona.
18. Max Meyer – Ameorodheshwa wa 78. kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 2 kutoka klabu ya Schalke ambaye amekamilisha pasi asilimia 92% msimu huu anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu huku Arsenal na Liverpool zikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Ujerumani
47. Holger Badstuber – Anaorodheshwa wa 72. Beki huyo wa zamani wa Bayern mwenye umri wa miaka 29 anakaribia kukamilisha kandarasi yake ya mwaka mmoja katika klabu ya Stuttgart.
Mbali na majera ni miongoni mwa wachezaji wenye pasi nzuri zaidi katika ligi ya Bundelsiga . Lazio ni miongoni mwa timu zinazomnyatia.
32. Yohan Cabaye – Amorodheshwa wa 75. kiungo huyo wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 32 bado anaonyesha mchezo mzuri kwa pasi zake murua mbali na kuharibu pasi za upinzani- swala ambalo linaweza kuchochea kupewa kandarasi mpya katika klabu hiyo.
41. James Collins – Ameorodheshwa wa 73. West Ham haijakuwa na msimu mzuri , lakini beki huyo mwenye umri wa miaka 34 huonyesha thamji yake anapokuwa vizuri. West Ham imeshinda asilimia ya mechi 34 anapocheza ikilinganishwa na asilimia 19% wakati anapowekwa benchi.
Mchezaji mwengine ambaye amekamilisha kandarasi yake lakini hayuko katika orodha ya CIES

No comments:

Post a Comment