TIMU YA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI AUSTRALIA YAREJEA MIKONO MITUPU - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 18, 2018

TIMU YA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI AUSTRALIA YAREJEA MIKONO MITUPU


 Kiongozi wa Msafara wa wachezaji waliyokwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia ambaye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na kwa waandishi wa habari (hawapo picha)kuhusu hali ya mashindano pamoja na suala la mchezaji mmoja kutoroka kambini  mara baada ya kuwasili nchini leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa Jijini Dar es Salaam.

 Bondia Selemani Kidunda (wa kwanza) akiwasilini leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea nchini Australia ambapo alikwenda kwa ajili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola  nyuma yake ni Bondia mwenzie Haruna Swanga.
 Mwanariadha wakike Bi.Sara Ramadhani akiwa amewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini Australia ambapo alikwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola na ameshika nafasi ya tisa katika mbio za Kilometa 42.
Kapteni wa Timu ya wachezaji waliyokwenda nchini Australia katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw.Masoud Mtalaso (kulia) akirejesha bendera aliyokabidhiwa wakati wanakwenda katika mashindano kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge (kushoto) mara baada ya kurejea nchini leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment