MLIPILI MCHEZAJI BORA SIMBA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 16, 2018

MLIPILI MCHEZAJI BORA SIMBA


Beki Yusuph Mlipili ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo kwa Simba dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Mlipili ameshinda kufuatia kura zilizopigwa na mashabiki wa timu hiyo zilizopigwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter na Instagram) za Simba.

Mchezaji huyo amekuwa bora huku timu yake ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wajelajela hao wa Mbeya.

Ushindi huo umeifanya Simba izidi kunusa ubingwa wa ligi kwa kufikisha pointi 58 kwenye msimamo msimu huu.

No comments:

Post a Comment