ZANZIBAR YAONDOLEWA CECAFA SABABU YA VIJEBA, YAPIGWA RUNGU KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 16, 2018

ZANZIBAR YAONDOLEWA CECAFA SABABU YA VIJEBA, YAPIGWA RUNGU KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Karume Boys, kimeondolewa katika mashindano ya CECAFA yanyofanyika nchini Burundi.

Timu hiyo imeondolewa kutokana na kupeleka wachezaji 12 waliozidi umri kitu ambacho ni kinyume na taratibu za mashindano.

Mbali na kuondolewa, Karume Boys imepigwa faini kulipa kiasi cha dola za kimarekani 15,000 ikiwa ni pamoja na gharama za tiketi huku ikifungiwa kushiriki mashindano kwa mwaka mmoja.

Hivi karibuni kikosi hicho kilifanyiwa mabadiliko wakati kikiwa kambini baada ya kubainika kuwa baadhi ya wachezaji walikuwa wamezidi umri, lakini imegundulika tena kuna baadhi hawana umri sahihi baada ya kuwasili Burundi.

Ethiopia nayo imekuwa ni miongoni mwa timu zilizopigwa faini hiyo ya USD 15,000 baada ya wachezaji kadhaa kuzidi umri pia. 

No comments:

Post a Comment