MBAO WAMEISHAONA KINACHOWAMALIZA, MWENYEKITI HUYU HAPA... - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 9, 2018

MBAO WAMEISHAONA KINACHOWAMALIZA, MWENYEKITI HUYU HAPA...

Klabu ya Mbao FC ambayo inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza michezo 22 na kufanikiwa kuvuna alama 19, imeweka wazi sababu kubwa zilizoiponza ikapata matokeo mabovu katika mechi za mzunguko wa pili ambazo walicheza.

Mwenyekiti wa Mbao, Soly Njashi, alisema kuwa lengo la Mbao siyo kufanya vibaya kwani wanafanya kila jitihada kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa ila kuna mambo ambayo hayapo sawa yanawaliza kwa kasi ya ajabu.

“Ratiba kwetu sio rafiki kwani ipo wazi kabisa tunasafiri umbali mrefu kufuata timu, wachezaji wanachoka tulitoka Njombe bila mapumziko safari ilikuwa ngumu tumecheza na Njombe kisha Mbeya, wakafuata Azam kwa ratiba hii hakuna uwezo wa kushinda, hapo safari ni ngumu.

“Maandalizi yanakwenda vizuri, wachezaji wapo vizuri, kinachotuponza ni uchovu wa wachezaji, wanatumia muda mwingi kusafiri kufuata timu kuliko kupumzika, hivyo wanaingia kwenye mechi ya ushindani wakiwa wamechoka, hilo lipo wazi kabisa halipingiki.

 “Tumejipanga vizuri tunarudi kwenye ubora wetu sasa maana mazoezi yanaendelea kila mchezaji ana morali anahitaji kufanya vizuri hivyo naamini kila kitu kitakuwa sawa maana ligi ya sasa imepamba sana moto, bado tuna nafasi ya kuonyesha uwezo,” alisema.

No comments:

Post a Comment