HARRY KANE ANAAMINI ATAMPIGA CHINI SALAH - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 9, 2018

HARRY KANE ANAAMINI ATAMPIGA CHINI SALAH


Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia msimu huu. 

Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 24 msimu huu. Hata hivyo, ameachwa nyuma na Salah ambaye ni raia wa Misri kwa mabao matano.

Kane, 24, anapigania kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya England kwa misimu mitatu mtawalia.

"Naamini ninaweza kufanya hivyo. Bado kuna mechi zilizosalia kuchezwa," Kane amesema.
"Lazima niendelee kuangazia uchezaji wangu. Siwezi kudhibiti anachofanya yeye.

"Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kuishinda buti ya dhahabu tena na nitaendelea kutia bidhii kuanzia sasa hdi mwisho wa msimu."

Kane ambaye amekuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mfuu amerejea kucheza baada ya kupona.

Mshindani wake Salaha, 25, hata hivyo hakucheza debi ya Merseyside Jumamosi kutokana na jeraha la mtoki alilopata akichea Liverpool mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambapo waliwalaza Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza robofainali.

Kane ana nafuu kidogo ukizingatia kwamba Spurs wamesalia na mechi sita za kucheza Ligi Kuu lakini Liverpool wana mechi tano pekee.

Na huenda bado akafaidika zaidi katika kupunguza mwanya kati yake na Salah iwapo atahesabiwa bao la ushindi dhidi ya Stoke Jumamosi, ingawa kituo cha wasimamizi wa mechi cha Ligi ya Premia siku hiyo kiliamua kwamba Christian Eriksen ndiye aliyefunga bao hilo.

No comments:

Post a Comment