Na Alex Mwenda-Songea
Majimaji hii leo
wameweza kushinda ugenini dhidi ya Stend united kwa mabao 3-1.
Mabao ya Lucas kikoti,
Peter Mapunda na Jerson Tegete likiwa ni bao lake la pili la msimu huu wa VPL,
lakini ni bao lake la tatu tangu asajiliwe na Majimaji.
Mara ya mwisho
majimaji kupata ushindi alipata dhidi ya Stend united uwanja wa majimaji mjini
songea 2-1.
Tegete anakuwa sawa
kwa magoli na ndugu yake Ngassa ambaye pia na mabao mawili, juzi tuu kafunga
pia leo Tegette kafunga. Peter Mapunda ni goli lake la 4 msimu huu, kinara ni
Marcelo Kaheza Boniventure mwenye goli 9.
Kwa matokeo haya
Majimaji wanapanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya 15 kwa alama 19, nyuma ya
Njombe Mji wenye alama 18 baada ya hii leo kupoteza mbele ya Mbao fc.
Majimaji watashuka
tena dimbani tarehe 15 mwezi huu kuwavaa Mbao fc katika uwanja wa Ccm Kirumba
mkoani Mwanza, kasha kuwasubili Ruvu shooting tarehe 28 mwezi huu, na tarehe 5
mwezi wa 5 watawakaribisha Mtibwa.
No comments:
Post a Comment