Kutinyu wa Singida United huyooo Yanga.. Ishu kamili hii hapa - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 4, 2018

Kutinyu wa Singida United huyooo Yanga.. Ishu kamili hii hapa

Image result for KUTINYU
Kutinyu wa Singida United huyooo Yanga.. Ishu kamili hii hapa Kuna uwezekano mkubwa Wa Klabu ya Yanga kumnasa mchezaji wa Singida United Tafadzwa Kutinyu kwani kuna taarifa za Uhakika kuwa vigogo wa Yanga wako tayari kuhakikisha wananasa Saini ya Nyota Huyo.

 Kutinyu msomaji wa kwataunit alikuwa atue Yanga toka wakati wa Dirisha Dogo lakini Mambo hayakwenda sawa lakini kwasasa moja wa Kigogo wa Yanga ametuthibitishia kuwa huenda Dirisha Kubwa Akatua Jangwani.

“Ni kweli tumekuwa tukimfatilia Kutinyu kwa muda sasa na Tuko tayari tuwape Donald Ngoma ambaye Kocha wao Pluijm anampenda ili sisi tumnase Kutinyu ” Alisema moja ya Kigogo kutoka Yanga. KUTINYU alikuwa moja ya wachezaji walioisumbua sana Safu ya Ulinzi ya Yanga katika mchezo wa Robo Fainali kombe La Azam Sports Federation Cup.

No comments:

Post a Comment