IFAHAMU ARSENAL VIZURI NA HISTORIA YAKE - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 2, 2018

IFAHAMU ARSENAL VIZURI NA HISTORIA YAKE

Image may contain: 4 peopleWORLDWIDE FOOTBALL
MADINI ADIMU KUHUSU KLABU YA ARSENAL
1. Arsena iliitwa jina la utani la THE GUNNERS na kikundi cha watengeza mitumbwi cha Woolwich Arsenal mwaka 1886
2. Arsenal ndiyo klabu pekee ambayo haijawahi kushuka daraji kwa pale england tangu ilipopandishwa daraja (top flight football) msimu 1919/1920
3. Arsenal ndiyo klabu pekee kwa England iliyofanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya England (EPL) bila kufungwa. Ilifanya ivo msimu wa 2003-04. Kwa kushinda michezo 26, na kudroo michezo12.
4. Arsenal ndiyo klabu pekee katika ligi ya uingereza kuwahi kukabidhiwa kombe la ligi la dhahabu. Wakitunukiwa kombe hilo mwaka 2003/04 baada ya kuchukua bila kupoteza mchezo wowote.
5. Kocha wa arsenal Arsene Wenger ndiye kocha wa kwanza wa kigeni (non UK) kuchukua kombe la ligi kuu ya EPL. Alifanya hivyo mwaka 1997/98
6. Arsenal ni klabu ya kwanza ya England kuwahi kuvifunga vilabu vya Real Madrid, Bayern Munich n AC Milan katika viwanja vyao vya nyumbani.
7. Arsenal ni klabu pekee ya England iliyoweza kuvifunga vilabu vya Inter milan (2003) na AC Milan (2008, 2018) katika viwanja vyao vya nyumbani.
8. Arsenal ilikua klabu ya kwanza nchini uingereza kushinda makombe ya ligi (siyo epl haya ni CARLING/CAPITAL ONE CUP) na kombe la FA katika mwaka/ msimu mmoja. Walifanya ivo mwaka 1993.
9. Arsenal ndiyo klabu inayoshikiria record ya kucheza michezo mingi ya ligi ya mabingwa ulaya UCL bila kuruhusu goli (keep clean sheet) kwa muda mrefu. Walicheza mechi 10 yaani dakika 995 bila kuruhusu goli.
10. Arsenal vs Shelfield united iliyochezwa mwaka 1927 ndiyo mechi ya kwanza ya ligi ya uingereza kutangazwa/kurushwa kwenye redio.
Na Mechi kati ya timu ya kwanza ya arsenal na timu ya pili (arsen first team vs arsenal reserve team) ndiyo mechi ya kwanza kurushwa kwenye televisheni mwaka 1937.
KAMA ULIKUA HUJUI👇👇
Arsenal ndiyo klabu ya kwanza nchini uingereza kuvaa jezi zenye majina.

LikeShow more reactions

No comments:

Post a Comment