WATANGAZAJI WANAOPENDWA NA WANAOONGOZA KWA KUSIKILIZWA ZAIDI MKOANI RUVUMA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 28, 2018

WATANGAZAJI WANAOPENDWA NA WANAOONGOZA KWA KUSIKILIZWA ZAIDI MKOANI RUVUMA


Image may contain: 1 person, sitting
10. NEEMA MLIGO KEYFM RADIO 90.5 kipindi BAHASHA YA JAMII
Kwa mujibu wa wadau wa mkoa wa Ruvuma wametolea maoni kuwa huyu mwanadada ni kati  ya waonaomfuatilia zaidi kutokana na umaili wake awapo katika maiki na elimu anayoitoa, lakini mvuto zaidi ni juu ya sauti yake maridadi kabisa.


Image may contain: 1 person, closeup
9.STELAH KHAMIS KEYFM RADIO 90.5 kipindi MTAA KWA MTAA
Amekuwa akiwavutia wengi sana kutokana na uhodari wake wa sauti nzuri na kujiamini imemfanya awe kati ya watangazaji wanaofuatiliwa zaidi na wadau wengi.


Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting
8.TITTO SOVELLA kipindi MTAA KWA MTAA
Uhodari wake katika sauti na kuwapa wananchi udambwiudambwi wa habari za kijamii imempa zaidi nafasi kuwa kati ya watangazaji wanaopendwa na kuwa na mvuto zaidi kwa wasikilizaji hasa akina mama.

Image may contain: 1 person, standing and shoes
7.KISS DAVLON KEYFM RADIO kipindi BACK TO SCHOOL
Amekuwa balozi mzuri wa wanafunzi ukanda huu wa nyanda za juu kusini kutokana na umahiri wake wa kutengeneza mijadala ambayo imekuwa ikiwavutiwa wengi kuanzia wanafunzi hadi wazazi kuweza kumsikiliza, pia sauti yake murua ya kuvutia na ya kujiamini imemfanya kuwepo katika orodha hii ya watangazaji wanosikilizwa zaidi.

Image may contain: 4 people, people standing and outdoor
6.GIMMIE CHURCH BOY keyfm radio kipindi KEYBASE
Moja kati ya watangazaji bora kabisa wa vipindi vya burudani, amekuwa akifanya vizuri kwa mujibu wa wasikilizaji wa radio mkoani Ruvuma, staili yake ya uwasilishaji wa stori na swaga zake zimekuwa ni kivutio kwa wadada wengi zaidi.

Image may contain: 1 person, closeup
5.MR CLEVER kipindi BAHASHA YA JAMII
Amekuwa hodari zaidi hasa katika kuandika stori za matukio ambayo ni current, na umahiri wake zaidi upo katika dawati la habari akiwa kama mhariri.

Image may contain: 3 people, people smiling, people standing and outdoor
4.DANIEL MILLINGA kipindi KEYDRIVE
Sauti yake na jinsi anavyojiamini katika kipindi imemfanya kuwa kati ya watangazaji wanaofuatiliwa zaidi na raia wengi. Ubunifu wake wa vitu vipya kila siku unazidi kumpa umaarufu zaidi, bila kusahau kipindi chake cha GOSPEL MIRACLE kimeteka hisia za mashabiki wengi. Keydrive wapo pia ambao wanaofuatiliwa kama Rauph Mohammed na Wilfred Duncan.

Image may contain: 3 people, people on stage, people standing and outdoor
3.ALEX MWENDA Daady kipindi KEYSPORTS & CHOCOLATE LOVE
Unaweza kusema ndo mtangazaji anaeongoza kwa kusikilizwa na watu wengi zaidi mkoani Ruvuma. Vipindi vyake vya Michezo uhodari katika kuchambua habari za kisports, bila kusahau kutangaza mpira imemfanya ajijengee heshima kubwa saana. Lakini pia kipindi cha mapenzi usiku ndo anakozoa umaarufu wa jina lake huko kutokana na kuwa bora katika kufundisha jamii juu ya mambo ya mahusiano, bila kusahau jumapili katika kipindi cha Maisha ni safari. Huyu ndo mtangazaji anaeongoza kwa kusikilizwa zaidi kwa mujibu wa mitazamo ya watu.

Image may contain: 1 person, standing and outdoor
2.PRINCE WALTER kipindi KEYBASE
Moja kati ya vipindi bora sana vya burudani nyanda za juu ya kusini basi ni Keybase. Amekuwa hodari katika ubunifu na pia sauti yake kuwa kivutio kwa watu wengi zaidi sio watoto au wakubwa. Kubwa zaidi huyu ndie mtangazaji bora wa kiume mkoani Ruvuma kwa mwaka 2017.

Image may contain: 6 people, people standing, people on stage and outdoor
1.BERTHER PONERA MWANA WA NCHENJERE-KEYSPORTS
Mwanamke aliejaliwa sauti nzuri yenye mvuto na kinamchomfanya awe hapa kutokana na ubora wake katika kuhost kipindi cha michezo ambacho ni nadra sana kwa wanawake duniani kuona wakifanya. Na amekuwa akisikilizwa zaidi na kupendwa. Kubwa zaidi ni kwamba huyu ndie mtangazaji bora wa kike mkoani Ruvuma kwa mwaka 2017.

Picha hapo chini ya kumbukumbu wakati akikabidhiwa cheti cha pongezi
Image may contain: 2 people, people standing

DJ GANGISA
Image may contain: 1 person, sitting
Ni miongoni mwa madjs ambao mziki wake anaoupiga unakubalika zaidi

No comments:

Post a Comment