KAULI YA YANGA BAADA YA KUHUSISHWA USAJILI WA MCHEZAJI HUYU KUTOKA SINGIDA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 28, 2018

KAULI YA YANGA BAADA YA KUHUSISHWA USAJILI WA MCHEZAJI HUYU KUTOKA SINGIDA



Wakati Yanga ikiwa kwenye maandalizi ya kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United FC, taarifa za chini ya kapeti zinaeleza uongozi wa timu hiyo unataka kumsajili Mudathir Yahaya.

Yahaya anaichezea Singida United akitokea Azam FC kwa mkopo ambayo leo imetangaza kuwa mkataba wake umemalizika rasmi na yupo huru kwenda popote.

Kupitia kipindi cha michezo cha Radio One, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, amesema wao kama klabu hawajazungumza na mchezaji huyo.

"Sisi hatujazungumza na Yahaya, akili yetu inafikiria mchezo ujao wa FA dhidi ya Singida United" alisema.

Aidha Nyika ameeleza kuwa yeye hana majukumu ya kusajili mchezaji bila Kocha kuamua kuamua, na endapo kama itatokea anahitajika, atatimiza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment