NA ALEX MWENDA
Siri ya kipaji ni
mafanikio, na mafanikio huja kama unakitendea haki kipaji chako, na kipaji
chako huonekana kama unapewa nafasi ya kuonesha kipaji chako…..mmmh lisikutishe
hilo……..
Walimwengu humtambua
kama shujaa wa soka wa bara la Afrika kwani uwezo wake ni wakumfananisha na JAY
JAY OKOCHA, GEORGE WEAH, AL HAJI DIOF, mmh hata Mbwana Samatta huenda akawa
ananusa harufu yake.
Huyo sio mwingine ni
nyota wa Simba wa Afrika ambae alitamba na anaendelea kutamba katika ulimwengu
huu wa mchezo huu wa mpira wa miguu. Alizaliwa
tarehe 10.03.1981 katika mji wa Douala maarufu sana nchini Cameroon.
Kuna wakati mpaka
mama wa mchezaji huyu aliuza kila kitu kumsafirisha mwanae akatafute maisha
barani Ulaya. Kama sio huruma ya mama huyu tusingemfahamu SHUJAA WETU WA LEO NDANI
YA KEYSPORTS……
Alianza kufanya
mazoezi akiwa katika akademi ya Khadji sports, baada ya hapo alijiunga na timu
ya vijana ya Real Madrid katika mwaka 1997, na alikuwa mchezaji mwenye kipaji
cha pekee zaidi kutokana na kufanya mazoezi na timu ya pili ya Real Madrid.
Alishindwa kucheza Segunda B kutokana nayeye
kutoKUWA NA KIBALI cha kucheza soka barani Ulaya. Alitolewa kwa mkopo kuelekea
klabu ya Leganes iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la pili mnamo mwaka 1997-1998
na alicheza michezo 30 na kufunga magoli manne pekee.
Samuel Etoo alilejea
tena Real Madrid na kumalizia msimu wa mwaka 1998-1999. Katika mwezi januari
1999, alitolewa kwa mkopo kwenda Espanyol na hakuweza kucheza mchezo wowote
klabuni hapo.
Msimu uliofuata
katika dirisha la usajili majira ya joto alihamia ligi kuu laliga nchini
Hispania katika klabu ya Real mallorca
kwa mkopo, na alifunga magoli 6 katika michezo 19. Mwishoni mwa msimu Samuel
Etoo aliachana na Real Madrid na kusaini mkataba na Real mallorca kwa euro
milioni 4.4 kama ada ya uhamisho.
Katika msimu wake wa
kwanza alifunga magoli 11 katika ligi. Na kupewa sifa kede kede na aliekuwa
raisi wa timu hiyo Mateo Alemany kuwa staili ya mchezaji huyo kuwa ya kipekee
zaidi.
Aliisaidia Real
mallorca kufika fainali ya Copa del rey dhidi ya Recreativo de Huelva katika
mwaka 2003, mchezo ambao mallorca ilishinda mabao matatu kwa sifuri huku Etoo
akifunga mabao mawili katia mchezo huo.
Kwa muda wote ambao
Samuel Etoo aliichezea Mallorca aliweza kufunga mabao 54. mwaka 2004 katika
kipindi cha majira ya baridi alisaini klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho wa
euro 24 milioni baada ya makubaliano yaliyofanyika na timu za Real Madrid na mallorca, huku kipengele cha Madrid
kikiwekwa kuwa wakati wowote wakihitaji kumnunua waweze kamnunua.
Etoo alianza
kuichezea Barcelona katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Racing Santanda tarehe
29.08.2004, baada ya Barcelona kushinda laliga msimu wa mwaka 2004-2005. Akiwa
ametwaa ubingwa na wababe hao wa camp nou Etoo aliwaudhi mashabiki wa Real
Madrid baada ya kuposti Madrid, bastards, salute tha champions, kwa tafasisi ni
kwamba aliwaambia Madrid kuwa washamba na wanatakiwa kuheshimu mabwingwa.
Chama cha sheria na
hadhi na wachezaji nchini Uhispania The Royal Spanish Football Federation kilimtoza euro
12,000 kwa maneno yake na kuamriwa kuomba radhi kwa mashabiki kutokana na
matamshi aliyoyatoa. Kauli yake ilionekana kukerwa zaidi na maofisa wa Real
Madrid ambao walimkuza walimpokea akitokea barani Afrika nma kumkuza kisoka.
Alisaini
mkataba mpya na Fc Barcelona mnamo mwezi june 2005. Baada ya kukosa ufungaji
bora almaarufu PICHICHI TROPHY ambayo inatolewa na Laliga, Etoo alizidiwa na mshambuliaji wa Valencia David Villa katika
tuzo ambayo ilitolewa katika mchezo wa may 20, 2006. Na aliiwezesha Barcelona
kufunga mabao matano katika msimu wa mwaka 200-2006 michuano ya UEFA CHAMPIONS
LIGI.
Eto'o alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Uefa katika
nchi ambazo ni za ushindani barani Ulaya..
Alishinda pia tuzo ya mchezaji bora
wa Afrika katika msimu….Na alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa
wakiwania tuzo ya mchezaji bora na hakufanikiwa kushinda tuzo hiyo ambayo
historia bado imeshikiliwa na muafrika George Weah kutoka Liberia.
Huo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa safari ya Samueli Etoo.
TUZO BINAFSI
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
·
REKODI ALIZOWEKA
·
ETOO ana ndugu zake wawili
ambao ni kaka zake David na Etienne ambao wote ni wachezaji pia wa mpira wa
miguu.
Etoo ana watoto wane
Maelle, Etienne, Siena na Lynn. Alioa mke mnamo 6.julai.2007..Georgette ni mama wa
watoto Siena na Lynn ambao wote anaishi nao Paris nchini Ufaransa. Kwa hiyo
wewe mdada ambaye ulidhani Etoo hajaoa na kama una nafasi basi amejituliza kwa
bibie Georgette….
No comments:
Post a Comment