Tunapozungumzia suala la mashujaa ulimwenguni basi
tunawaangaza mashujaa wengi sana Chief Songea, Kinjikitile Ngware, Chief
Mkwawa, chief Milambo, Mwalimu Nyerere, Kwame Nkruma, tukija katika ngazi za
michezo wapo kina Stivin Mapunda, King Kibaden, Salvatory Edward, mtemi
Ramadhan na mashujaa wengi ambao walitamba katika ulimwengu wa soka hapa
Tanzania.
Turudi katika upande wa masumbwi wapo mabondia
wengi sana ambao walifanya vizuri katika mapambano hapo aaaah namkumbuka Snake
boy, Fransis Cheka, marehemu Thomas Mashari, nawakumbuka na mawandondi wengi
sana ambao walifanya vizuri sana.
Hapa mkoani Ruvuma tunao wanandondi wachache ambao
wanafanya vizuri katika ulimwengu wa mapigano, Mussa Omary, Roy Mbunda, lakini shujaa wa
Keysports kwa siku hii ya leo ni Benson Mwakyembe, uwiiiiii huyu jamaakama
angezaliwa marekani tungemfananisha na Froyd Mayweather, au hata Mohameid Ali..
Katika michezo yote hapa mkoani Ruvuma ambayo
ilikuwa inaitangaza vizuri mkoa wetu basi ni mchezo wa ngumi, hivi ninyi
viongozi wa chama cha ngumi hapa mkoani Ruvuma mnasimamia kweli kwa nafasi
mliyojiweka? inasikitisha sana kwa mtu kama Benson Mwakyembe mwanamasumbwi bora
sana hapa Ruvuma na Afrika mashariki yote
lakini macho yenu kama hayamtazami hivi na ubora wake, leo hii Benson
Mwakyembe ni mtu wa kufanya kazi za kukatisha watu tiketi kweli????
Mmesahau alivyoitangaza vizuri mkoa wa Ruvuma
katika masumbwi, mnakumbuka alivyopata ushindi mbele ya Mkenya 2013,
mmesahau kabisa mara ya mwisho alipata
ushindi tena hapa hapa Ruvuma uwanja wa majimaji, yote hayo mmesahau na
mnachofurahia ni kuona kipaji cha kijana huyu kikiwa kinadidimia katika ardhi
isiyo na msaada…..
Ni aibu kubwa sana kwa chama cha ngumi mkoani
Ruvuma kushindwa kuwaandaa madondia haya wazuri, mnashindwa hata kutafuta
udhamini wa kusimamia mchezo huu??? kuna haja gani sasa ya kuwepo kwa chama cha
ngumi na kama kipo kinafanya kazi gani,,,,tuendelee kusubili tuu mpaka Kaike
promotions amwandalie pambano Benson Mwakyembe, apate matokeo mazuri Wanaruvuma
tujivunie…
Hapa ndo napowaza kwanini Alexx Mwenda anapenda
masumbwi lakini haingii kucheza na anabaki kuwa shabiki wa Antony Joshua ndipo
napopata majibu yake….Benson Mwakyembe wewe ndio shujaa wetu wa leo ndani ya
keysports tunaojua ngumi tunatambua uwepo mchango wako, na tunaomba makampuni
mbalimbali wajitokeze kudhamini mchezo huu wa masumbwi ili siku moja tuwaone
wanamasumbwi wetu katika ubora wa kimataifa…..
Usijutie Benson kuzaliwa Tanzania na kukulia arhi
ya Ruvuma, hata Alex Mwenda anatamani angezaliwa Marekani ambao wanajua namna
ya kuvitumia vipaji vya masumbwi, lakini apambane na hali yake kwasababu tayari
alishazaliwa hapa Tanzania……
Wanaruvuma kwa pamoja tushirikiane taasisi binafsi,
makampuni mbalimbali, wafanya biashara tuandae pambano katika mkoa wetu wa
Ruvuma, tusibaki kushabikia pambano la Fransisi Cheka na Abdalah Pazi Dulla
mbabe, kwa pamoja tunaweza…..
Huyu ndie Benson Mwakyembe
shujaa ambae anapotezwa na kipaji chake
katika ramani ya masumbwi
No comments:
Post a Comment