TANZANIA KUANZA NA HAWA HAPA KOMBE LA CHALLENGE - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, November 16, 2017

TANZANIA KUANZA NA HAWA HAPA KOMBE LA CHALLENGE

TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya.
Katika droo iliyopangwa leo mjini Nairobi, Kenya ambako michuano hiyo inafanyika kuanzia Desemba 3 hadi 17, mwaka huu, Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.
Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.
Image result for taifa stars
Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9  na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za
Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.
Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.

CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.
Wadhamini tofauti wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kipindi chote hicho, lakini taarifa zinasema kuanzia mwaka huu Televisheni namba moja Afrika Mashariki na Kati, Azam TV ndiyo wanakuwa wadhamini wapya ambao pia watakuwa wanarusha moja kwa moja michuano hiyo. 
Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.
Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.  

RATIBA CHALENGE 2017
Desemba 3, 2017
Libya vs Tanzania
Kenya vs Rwanda
Desemba 4, 2017
Burundi vs Ethiopia
Uganda vs Zimbabwe
Desemba 5, 2017
Zanzibar vs Rwanda
Kenya vs Libya
Desemba 6, 2017
Sudan Kusini vs Zimbabwe
Uganda vs Burundi
Desemba 7, 2017
Tanzania vs Zanzibar
Rwanda vs Libya
Desemba 8, 2017
Sudan Kusini vs Ethiopia
Zimbabwe vs Burundi
Desemba 9, 2017
Rwanda vs Tanzania
Kenya vs Zanzibar
Desemba 10, 2017
Sudan Kusini vs Burundi
Ethiopia vs Uganda
Desemba 11, 2017
Libya vs Zanzibar
Kenya vs Tanzania
Desemba 12, 2017
Uganda vs Sudan Kusini
Zimbabwe vs Ethiopia
Desemba 13, 2017
MAPUMZIKO
Desemba 14, 2017
NUSU FAINALI
Mshindi Kundi A Vs Mshindi wa Pili Kundi B
Desemba 15, 2017
Mshindi Kundi B Vs Mshindi wa Pili Kundi A
Desemba 16, 2017
MAPUMZIKO
Desemba 17, 2017
Fainali/Mshindi wa Tatu

No comments:

Post a Comment