Kunani kati ya Rich Mavoko na Nay wa Mitego? kauli hii yazusha utata - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, April 11, 2017

Kunani kati ya Rich Mavoko na Nay wa Mitego? kauli hii yazusha utata

Wakali wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Rich Mavoko & Nay wa Mitego  wamejikuta wakijibizana mitandaoni baada ya Mavoko kutupia picha na maneno yaliashiria ujio wa ngoma yake mpya wakati akisikilizia hali ya kisiasa hapa nchini kwa sasa.
Hitmaker huyo ameonjesha picha ya kile kinachoonekana kuwa ni video yake mpya na kuandika: “Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii #Showme”
(instagram post)
Baada ya Post hiyo Saa 18 baadaye, Nay wa Mitego naye akachukua picha ile ile aliyotupia Mavoko, aka-repost na kuandika huku akitamba kuwa ngoma pekee inayoweza kutusua kwa sasa ni ngoma yake ya Wapo. “NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI”.
(instagram post)
Baada ya kutoa maneno hayo, Nay alitumia fursa hiyo kwa kumuonya Diamond Platnumz kwa kumtumia salamu zilizosomeka hivi.. “MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWA SASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA”.

No comments:

Post a Comment