aba Levo ambaye ni diwani wa Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma
amefunguka maendeleo yake katika uongozi huo katika kipindi cha mwaka
mmoja tangu alipochaguliwa kukalia kiti hicho.
Akiongea katika kipindi cha Mega Mix cha Abood FM ya Morogoro, Baba
Levo amesema katika kipindi alichokaa katika uongozi huo tayari
amewasaidia wananchi wake kwenya Afya, elimu na miundombinu kwa asilimia
kubwa.
“Cha kwanza kabisa ni kufufua zahanati ambayo ilikuwa imekufa inawapa
mateso zaidi wananchi wa Mwanga Kaskazini wamekuwa wakilazimika
kutembea umbali mrefu kupata huduma za kiafya wakati kuna zahanati
katika kata yao. Kwahiyo nimeifufua na kuifanya iweze kutoa huduma kama
kawaida,” amesema.
“Kwa upande wa elimu nimeweza kumaliza matatizo hayo katika shule
zangu. Mimi nina shule tano katika kata yangu, kwahiyo shule tatu
nimefuta tatizo la madawati zimebakia katika shule mbili ambapo nina
nuhakika katika kumaliza mwaka huu na kwenyewe nitakuwa nimefuta tatizo
la madawati. Na pia nimeweza kupigania kupata walimu wa Sayansi katika
kata yangu, walimu wa sayansi wamekuwa tatizo kubwa siyo katika kata
yangu tu bali ni Tanzania nzima. Nimepambana nimeweza kupata walimu
takribani wanne wa sayansi,” ameongeza.
“Niliwaahidi wananchi wangu kuwajengea soko la jioni ambalo watakuwa
wanafanya shughuli zao kwa uhuru bila kubuguziwa kwa kuwa kutakuwa na
mwanga ambao utatokana na taa za sola zenye thamani ya shilingi milioni
35. Nashukuru mpaka sasa tumeshakamilisha kuweka taa imebakia tu
kusakafia chini ili mambo yaweze kwenda.”
Wakati huo huo kiongozi huyo amesisitiza kuwa kata yake ina matatizo
makubwa ya barabara, lakini tayari amepata barabara nne ambazo zinapita
katika mitaa ambayo ilikuwa haipitiki hapo mwanzoni.
Tuesday, April 11, 2017
New
Baba Levo ataja maendeleo aliyoyapeleka kwenye kata ya Mwanga
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment