Jeshi la Polisi Mkoa Ruvuma limelazimika kuwatawanya kwa Mabomu ya Machozi, Baadhi ya wananchi wenye hasira kali wa Kata ya Mshangano Mtaa wa Namanyigu Manispaa ya Songea waliokusanyika na kuwalazimisha Alex Maundi na Mkewa kuchimba kaburi, kisha kuwataka wamzike mtoto wao mbae wanadaiwa kumuua kwa imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea leo majira ya Saa Tatu Asubuhi baada ya Kijana Daniel Mahundi anaekadiriwa kuwa na Umri wa Miaka 30 kufariki Dunia usiku wa Tarehe 19/2 mwaka huu 2017 kwa kile kinachoelezwa kuwa aliugua jino na kisha kupoteza maisha.
Wawili hao inaelezwa kuwa walitakiwa kupewa adhabu ya kuchimba kaburi,
kisha kumbeba Marehemu na wakamzike wao wenyewe kwa madai kuwa wao ndio
huenda wamesababisha kifo chake kwa imani za kisharikina .
Aidha wananchi waliokuwa katika eneo la tukio wanaeleza kuwa hii ni zaidi ya mara ya tatu watu hao kuhusika na tuhumza kama hiyo na kote walikoisha waliondolewa na wananchi.
Jeshi la Polisi limelazika kuondoka na Mwili wa Marehemu na kuupeleka Hospitali ya Mkoa na watu hao wawili wanashikiliwa na jeshi hilo kwa Mahojiano zaidi.

No comments:
Post a Comment