Vijana hao wa Antonio Conte, ambao watawakaribisha United Stamford Bridge katika robo fainali Kombe la FA mwezi Machi, wamo mbele kwa alama nane katika msimamo wa ligi na bado wamesalia na michezo 13.
Chelsea waliendelea na makali yao kwa kuchapa Wolves 2-0 katika raundi ya tano Kombe la FA, huku United wakitoka nyuma na kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Blackburn.
''Kombe la FA ni kitu muhimu kwao,'' amesema meneja wa zamani wa Blues, Mourinho.
"Chelsea wanaweza kuangazia vyema michuano ya FA, kwa fikira zangu kwani ni mabigwa na hawana michuano mingine inayowatatiza. Kombe la FA ni muhimu kwao.2
Katika msimu wa kwanza kwa meneja Mourinho uwanjani Old Trafford, ameongoza klabu hiyo kuwa miongoni mwa timu 32 bora katika ligi ya Europa, ambapo kwa sasa wamo kifua mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya Saint- Etienne ya Ufaransa .
United wanashikilia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Premia.


No comments:
Post a Comment