Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema uamuzi huo unatokana joto la pambano hilo hivyo kuamua kutotaja jina la mwamuzi kwa usalama wake.
” Tunaweza kumtaja siku moja au hata siku yenyewe ya mchezo. Hii ni kumuepushia na mihemko, anapoishi kuna mashabiki wa Simba na Yanga jambo ambalo linaweza kuwa kero na presha kwake kuelekea pambano hilo.” Amesema Alfred.
Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi ya wiki ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Pambano lililopita la watani wa jadi lilichezeshwa na Martin Saanya na kuzua utata kadhaa ikiwemo kadi nyekundu kwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude ambayo hata hivyo ilikuja kufutwa.

No comments:
Post a Comment