Kamati hio ya TFF itazungumzia kesi hio kufuatia ombi la Yanga kuomba kupitiwa upya kwa mwenendo mzima wa utaratibu na kanuni zilizopelekea kuamliwa kuwalipa wapinzani wao Simba fidia ya shilingi milioni 50 pamoja na faini ya shilingi 3 kwa kuvunja kanuni katika kumsainisha mkataba Kessy kutokea Simba.
Baada ya uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji uliotolewa katikati ya Disemba mwaka jana, Yanga hawakuridhika na uamuzi na hivyo kuwasilisha ombi la kutazamwa kwa mwenendo mzima wa kesi.
Simba waliishtaki Yanga kwa kumsainisha mkataba kinyemela Kessy na pia wakamshtaki Kessy kwa kuvunja mkataba na klabu hio.
No comments:
Post a Comment