Mwamuzi anayeaminika kuwa bora zaidi kwa sasa, Mark Clattenburg anajiuzulu kuchezesha mechi za Ligi Kuu Uingereza ili atimkie Saudia Arabia.
Clattenburg ameamua kujiengua katika Ligi yenye mvuto ili apate fursa ya kufanya kazi nchini Saudia Arabia kama mkuu wa waamuzi nchini humo.
Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 41, msimu uliopita alichezesha fainali ya Euro 2016, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA.
Hatua ya Clattenburg kutimkia Saudia Arabia inakuja ikiwa ni siku 11 tu baada ya mwamuzi mwingine wa Uingereza Howard Webb kujiuzulu kama mkuu wa waamuzi nchini Saudia Arabia.
Amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye vipengele vya kuongezwa na anatarajiwa kuachana rasmi na kuchezesha Ligi Kuu Uingereza kabla ya mechi za raundi ya 25.
Majukumu makubwa ya Clattenburg yatakuwa ni kuboresha na kuimarisha uamuzi nchini Saudia Arabia na pia atakuwa akichezesha baadhi ya mechi za Ligi Kuu nchini humo.
No comments:
Post a Comment