MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta jana ameshindwa kuisaidia timu
yake, KRC Genk kupata ushindi nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya
1-1 na Charleroi SC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji
Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji.
Dakika
45 za kwanza zilimalizika bila mabao na kipindin cha pili, wenyeji Genk
wakatangulia kwa bao la penalti la Leandro Trossard dakika ya 84, kabla
ya Stergos Marinos kuiswazishia Charleroi SC dakika ya 86.
Mbwana Samatta alipambana sana, lakini akashindwa kuipa ushindi Genk nyumbani
Samatta
jana alicheza mechi yake ya 43 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana,
18 msimu uliopita na 25 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 24 tu
ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 13 msimu huu.
Mechi
19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu,
wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu
huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu
uliopita.
Kikosi
cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Colley, Brabec/Castagne dk67,
Berge, Malinovskyi/Boetius dk77, Pozuelo/Naranjo dk88, Trossard, Authors
na Samatta.
Charleroi
SC: Penneteau, Martos, Harbaoui, Diandy, Benavente/Hendrickx dk56,
Baby, Mata/Marinos dk79, Dessoleil, Marcq, N'Ganga na Bedia/Fall dk88.
Monday, February 20, 2017
New
SAMATTA ASHINDWA KUIBEBA GENK NYUMBANI, YALAZIMISHWA SARE 1-1
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment