Kweli nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema
ukistaajabu ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa
Mzee Willy Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada
ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.
Hehehe, Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata
tamaa, Je ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka
hiyo 60, hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy
aliupanga huo muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo.
Wanandoa hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai
kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa
wakitembea kwa fimbo.
Aidha Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya
MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura
hakumsaliti. “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara
amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.”
Kwa upande wake Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake
kama ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo, huku akidai kuwa
alimpenda sana Kinyua na kwamba walikuwa wakiishi kwa imani.
Monday, February 20, 2017
New
Mzee wa miaka 98 aoa bibi wa miaka 88 baada ya kuishi wote miaka 60
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MAHUSIANO
Labels:
MAHUSIANO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment