Nahodha wa timu ya faifa ya Tanzania Mbwana Samatta ametoa fursa kwa wadah kushauri chochote ambacho kinaweza kuifanya Stars ifuzu michuano ya AFCON 2019.
Kupitia ukurasa wake wa instagram na twitter, Samatta ame-post ujumbe wa kuomba ushauri.
“Hivi ukipata nafasi ya kushauri chochote ambacho kinaweza kuifanya ‘taifa stars’ kupata tiketi ya AFCON mwakani inadhani ungeshauri jambo gani? Nini kifanyike? Sina maana ushauri utafatwa au la lakini tuongelee tu hili jambo hapa. Lets start.”
Stars ipo Kundi L kwenye mapambano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya kucheza mechi moja.
No comments:
Post a Comment