Fainali ya NBA: Golden State Warriors waendeleza ubabe kwa Cavaliers - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, June 4, 2018

Fainali ya NBA: Golden State Warriors waendeleza ubabe kwa Cavaliers


Timu ya kikapu ya Golden State Warriors imefanikiwa kushinda fainali yake ya pili ya NBA dhidi ya Cleveland Cavaliers.
Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo kwenye uwanja wa Oracle Arena, California, Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 122 dhidi ya 103 vya Cleverland.
Stephen Curry amekuwa nyota wa fainali hiyo ya pili kwa upande wa Warriors baada ya kushinda vikapu 33 huku Kevin Durant akishinda vikapu 32 na kutoa rebounds 9 na assists 7.
Wakati huo huo Lebron James wa Cavaliers aliongoza kwa kutoa assists 13 katika fainali hiyo na kushinda pointi 29.

No comments:

Post a Comment