(VIDEO) SHUHUDIA YANGA WALIVYOTUNGULIWA NA WAARABU KOMBE LA SHIRIKISHO Harun Habari Za Kimataifa - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, May 7, 2018

(VIDEO) SHUHUDIA YANGA WALIVYOTUNGULIWA NA WAARABU KOMBE LA SHIRIKISHO Harun Habari Za Kimataifa


Yanga imeanza vibaya katika Kombe la Shirikisho Afrika kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 katika mchezo wao wa kwanza wa makundi dhidi ya USM Alger ya Algeria.
Yanga ikicheza ugenini bila nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza ilianza kuruhusu bao la kwanza dakika ya nne lakini hadi kipindi cha kwanza kina malizika walikuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Yanga ikaruhusu bao la mapema ndani ya dakika 10 za kwanza, wakati mchezo ukiwa kwenye muda wa nyongeza beki wa Yanga, Andrew Vicent alichezea faulo ndani ya eneo la 18 na hivyo kuwa penati ambapo kipa wa USM Alger aliifungia timu yake bao la nne.
Matokeo ya mechi nyingine za Kundi D, Rayon Sports imetola sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Kwa maana hiyo, USM Alger inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu ikifuatiwa  na Gor Mahia pamoja na Rayon Sports zenye poini mojamoja baada ya kila timu kucheza mechi moja.

No comments:

Post a Comment