DARMIAN BLIND WAWEKWA SOKONI MANCHESTER UNITED - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, May 2, 2018

DARMIAN BLIND WAWEKWA SOKONI MANCHESTER UNITED


Manchester United wapo tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji wao wawili Daley Blind na Matteo Darmian majira ya kiangazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.
United waliamua kutumia kipengele cha kumuongeza Blind mkataba mmoja zaidi mwezi Februari ili kuondoa uwezekano wa beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu.
Blind amecheza mara 16 msimu huu kwa United , lakini hajaanza kikosi cha kwanza katika mechi ya Ligi kuu ya Uingereza tangu Agosti 16.
Blind mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na United akitokea Ajax kwa dau la Pauni Milioni 13 mwaka 2014 alikuwa anakaribia kujiunga na AS Roma mwezi januari kuziba nafasi ya Emerson Palmieri aliyehamia Chelsea .
Darmian, yeye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa na hapo awali alikuwa akiwindwa na vilabu vya Roma na Napoli kwenye dirisha la usajili la Januari.
Beki huyo wa kimataifa wa Italia amecheza mar 15 msimu huu ndani ya Old Trafford , na mara 6 kati ya hizo ni mechi za Ligi kuu ya Uingereza. Darmian alijiunga na United kwa dili la Pauni Milioni 13 mwaka 2015 kutoka Torino.

No comments:

Post a Comment