Yanga Ubingwa Msimu Huu Huenda Ikawa Ndoto, Hizi Hapa Sababu Zinazoweza Kuwazuia Kutwaa Ubingwa.. - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 9, 2018

Yanga Ubingwa Msimu Huu Huenda Ikawa Ndoto, Hizi Hapa Sababu Zinazoweza Kuwazuia Kutwaa Ubingwa..

images%2B%252820%2529
LICHA ya ubingwa wa ligi kuu ya VPL, kuwa kwenye mabano, lakini Yanga ina nafasi finyu ya kutetea taji hilo, kutokana na sababu zifuatazo.

Katika mechi 21 ambazo Yanga wamecheza wamefanikiwa kupata pointi 46, mabao 38 na watani wao Simba kwa mechi 21 wana pointi 49 na mabao 51.

Endapo Simba ikishinda mechi zilizosalia basi Yanga, itakosa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, lakini zifuatazo ni sababu zilizochangia timu hiyo kupunguza makali yake.

Majeraha

Asilimia kubwa ya nyota ambao walikuwa nguzo kwenye kikosi cha kwanza, kilichopelekea msimu uliopita kuchukua ubingwa wa ligi hiyo, wanasumbuliwa na majeraha.

Mastaa hao ni Amissi Tambwe , Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Yohana Mkomola ambaye anacheza msimu kwa mara ya kwanza na Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye anacheza na kupumzika.

Ukata

Kukauka kwa pesa ndani ya timu hiyo ni sababu inayopelekea kuchelewa kulipa mishahara kwa wakati, kitendo ambacho kinaondoa morali ya kujituma.


Kukosa pesa pia kunawanyima uhuru wa kuchagua kambi za kuwaweka wachezaji wao kwa maandalizi ya mechi mbalimbali zinazokuwa mbele yao.

Kocha

Mzambia George Lwandamina alipokea kijiti cha Hans Pluijm aliyeajiriwa na Singida United, iliowatoa hatua ya robo fainali ya Kombe la FA, tangu aanze kuinoa Yanga, inakosa morali na kujituma kama ilivyokuwa awali.


Imebakia kuonekana uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, timu haichezi kitimu kama ilivyokuwa kwa Pluijm.

Mabao

Yanga msimu uliopita ilichukua ubingwa kwa kuizidi Simba mabao, ila pointi zilikuwa sawa, wakati huo walikuwepo washambulia hatari kama Ngoma, Tambwe na Simon Msuva aliyekuwa anashambulia kutokea pembeni.

Msuva anacheza soka la Morocco, lakini kwa Ngoma na Tambwe, walikosekana kwa muda mrefu katika ligi kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Posho

Kupungua kwa posho ni sababu inayowafanya wachezaji kukosa ari ya kujituma, kujua mwisho wa dakika 90 kuna kifuta jasho nje ya mshahara.


Lakini posho ni adimu ama hazijawa kwa ukubwa ule waliozoea kipindi ambacho Yusuph Manji ni mwenyekiti ndani ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment