Wakuu wa waamuzi watumiwa risasi kwa bahasha Italia - ALEX MWENDATZ

Breaking

Friday, April 6, 2018

Wakuu wa waamuzi watumiwa risasi kwa bahasha Italia

Ciro Immobile is sent off playing for Lazio
Maafisa watatu wakuu wa chama cha waamuzi Italia wametumiwa risasi katika kinachoonekana kama jaribio la kuwatisha kuhusu maamuzi uwanjani.
Rais wa chama hicho Marcello Nicchi amesema mwenyewe ametumiwa risasi zikiwa kwenye bahasha, sawa na naibu rais wa chaam hicho Narciso Pisacreta na afisa anayewachagua waamuzi Nicola Rizzoli.
Polisi wanachunguza kisa hicho.
Nicchi pia ameshutumu tamko la karibuni la mwanahabari mmoja wa runinga ambaye alidai kwamba waamuzi walikuwa "wametangaza vita dhidi ya raia".
"Kuna mwanahabari aliyetangaza akiwa hewani: 'Wametangaza vita dhidi ya raia na katika vita huwa haupulizi kipenga, unafyatua risasi. Lazima uwafyatulie risasi waamuzi na usiwaruhusu watoe uamuzi," alisema.
"Haya ndiyo matokeo."
Mwezi jana, mamia ya mashabiki wa Lazio waliandamana katika makao makuu ya Chama cha Soka cha Italia wakidai kwamba timu yao imekuwa ikionewa sana kutokana na makosa ya waamuzi na teknolojia ya kuwasaidia waamuzi (VAR) msimu huu.
Serie A ni moja ya ligi za Ulaya ambapo teknolojia ya VAR inafanyiwa majaribio.
Fifa iliidhinisha matumizi ya VAR katika Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu mwezi Machi.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa teknolojia hiyo kutumiwa kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment